Soko la watumwa

Soko la watumwa ni mahali ambapo watumwa wananunuliwa na kuuzwa. Masoko haya yakawa ni jambo muhimu katika historia ya utumwa, hasa katika biashara ya utumwa wa Kiarabu na biashara ya watumwa wa Marekani.

soko la watumwa zanzibar

Katika utawala wa Ottoman wakati wa karne ya 14, watumwa walikuwa bidhaa ya biashara katika maeneo maalum ya wauzaji ambayo yaliitwa "Esir " au "Yesir. kulikuwa na watumwa wa umri wote na jinsia zote, walikuwa uchi kabisa ili wanunuzi waweze kuwakagua.

Kuanzia miaka ya 1800 hadi 1890, kati ya watumwa 2500050000 wa kibantu waliletwa ili kuuzwa katika soko la watumwa la Zanzibar kwenda pwani ya Somalia. wengi wa watumwa hao walitoka katika makabila ya Wamakua, Wanyasa, Wayao, Wazaramo na Wazigua ambao ni makabila ya Tanzania, Msumbiji na malawi.