Stabat Mater (sanaa)
Stabat Mater katika sanaa ni aina ya michoro na sanamu za Yesu Msulubiwa ambamo mama yake huonyeshwa amesimama imara chini yake kadiri ya Injili ya Yohane 19:25. Kwa kawaida Bikira Maria huchorwa upande wa kulia, huku mtume Yohane akiwa amesimama kushoto.
Maria anaonekana tofauti na michoro na sanamu aina ya Pietà ambamo mara nyingi amezidiwa na uchungu hata kutaka kuzimia.
Jina hilo la Kilatini linamaanisha "Mama alikuwa amesimama" na linatokana na lile la sekwensya maarufu "Stabat Mater" inayotumika kati ya masomo ya Misa siku ya Bikira Maria wa Mateso, tarehe 15 Septemba.
Picha
hariri-
Gentile da Fabriano, 1400–1410 hivi
-
Rogier van der Weyden, 1460 hivi
-
Pietro Perugino, 1482 hivi
-
Gabriel Wuger, 1868
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Stabat Mater (sanaa) kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |