Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar

Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (kwa Kiingereza: Zanzibar International Film Festival, kifupi: ZIFF, pia hujulikana kama Festival of the Dhow Countries) ni tamasha la kila mwaka la filamu linalofanyika Zanzibar, Tanzania. Imeelezwa kuwa tukio kubwa zaidi la kitamaduni katika eneo la ukanda wa Afrika ya Mashariki. ZIFF ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka wa 1997 ili kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na mambo mengine ya kiutamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa kikanda.[1]

Tamasha la Filamu

hariri

Tamasha la kila mwaka la sanaa na tamaduni mbalimbali ni shughuli kuu ya ZIFF; tamasha hilo huadhimisha sanaa na tamaduni za bara la Afrika, Nchi za Ghuba, Iran, India, Pakistani na visiwa vya Bahari ya Hindi, kwa pamoja hujulikana kwa jina la nchi za Dhow. Sehemu kuu ya tamasha ni programu ya filamu inayojumuisha maonyesho ya ushindani na yasiyo ya ushindani. Filamu na video mbalimbali hushindania tuzo.[2]

Ingawa filamu za ushindani ni ambazo uzalishaji wake unahusiana na nchi za Dhow tu, programu ya tamasha inajumuisha filamu na video kutoka duniani kote zinazozungumzia mada zinazoakisi mambo ya ndani ya nchi za Dhow. [3]Shughuli na matukio ya tamasha hili ni pamoja na makongamano, warsha, na maonyesho ya filamu bora zaidi za ndani na kimataifa. Tamasha kubwa la muziki pia hufanyika likishirikisha wasanii kutoka Tanzania pamoja na wanamuziki wa kimataifa.[4] Programu ya tamasha pia hujumuisha vipengele maalum, warsha na semina kuhusu jukumu la filamu katika jamii za vijijini, masuala ya wanawake pamoja na watoto na maendeleo ya vijana. [5]

Tamasha hili bila shaka ndilo tamasha kubwa zaidi la sanaa na utamaduni barani Afrika, na linaendelea kuongoza kama tukio linalovutia watalii katika eneo hili. ZIFF sasa inatoa Tuzo 12 za Kimataifa zinazotolewa na majaji 5 wa Kimataifa. Kila mwaka ZIFF huonyesha zaidi ya filamu 150 zinazotengenezwa Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya, Amerika Kusini, Marekani na Asia.[6]

 
Watazamaji mwaka 2013

Tamasha la ZIFF sasa linaendesha programu 15 katika siku 10 zinazojumuisha:

  1. Film Competition
  2. Film Workshops
  3. Opening and Closing Nights
  4. Film Outreach Projections
  5. Women panorama
  6. Children panorama
  7. Village panorama
  8. Festival of Festivals
  9. Soko Film
  10. Art and Exhibition
  11. Children Film panorama
  12. UNICEF Life skills Camps
  13. Children Peace camps
  14. Difficult Dialogues
  15. Historical and Cultural Village Tours[7]

Matukio hayo mengi hufanyika katika eneo la Ngome Kongwe na Bustani za Forodhani na huwa bure kwa umma.[8] [9]

  • Golden Dhow
  • Silver Dhow
  • Documentary
  • Short/Animation
  • East Africa Talent
  • ZIFF Jury Award
  • UNICEF Award
  • ZIFF Life Time Achievement Award
  • ZIFF Chairman Award
  • Sembene Ousmane Award
  • Signis Award
  • East Africa Region Talent
  • Signis Jury Award — Commendation
  • Verona Award

Washindi wa Golden Dhow

hariri
Year Filamu Muongozaji Nchi
1998 Maangamizi: The Ancient One[10] Martin Mhando, Ron Mulvihill Tanzania/Marekani
2000 Jinnah[11] Jamil Dehlavi Pakistan
2001 Bawandar (The Sand Storm)[12] Jagmohan Mundhra India
2004 Maargam (The Path) Rajiv Vijay Raghavan India (kwa Kimalayalam)
2005 Khakestar-o-Khak (Earth and Ashes)[13] Atiq Rahimi Afghanistan
2006 L'Appel Des Arenes (Wrestling Grounds)[14] Cheikh Ndiaye Senegal/Moroko/Burkina Faso/Ufaransa
2007 Juju Factory[15] Balufu Bakupa-Kanyinda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
2008 Ezra[16] Newton I. Aduaka Nigeria/Ufaransa
2009 Jerusalema[17] Ralph Ziman Afrika Kusini
2010 Themba[18] Stefanie Sycholt Afrika Kusini
2011 The Rugged Priest[19] Bob Nyanja Kenya
2012 Uhlanga[19] Ndaba Ka Ngane Afrika Kusini
2013 Golchereh[20] Vahid Mousaia
2014 Half of a Yellow Sun Biyi Bandele Marekani
2015 Wazi ?FM Faras Cavallo Kenya
2016 Watatu Nick Reding Kenya
2017 Noem My Skollie Daryne Joshua Afrika Kusini
2018 Supa Modo[21] Likarion Wainaina Kenya/Ujerumani
2019 Fatwa[22] Mohamed Ben Mahmoud Tunisia
2022 Vuta N’Kuvute[23] Amil Shivji Tanzania

Tanbihi

hariri
  1. "Tanzania Travel Guide - Festival of the Dhow Countries - Zanzibar". www.safari.co.za. Iliwekwa mnamo 2022-07-04.
  2. "Zanzibar International Film Festival (ZIFF)". www.zanzibartourism.go.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-17. Iliwekwa mnamo 2022-07-05.
  3. "ZIFF set to quench thirst of revellers and film lovers". The Citizen (kwa Kiingereza). 2022-06-17. Iliwekwa mnamo 2022-07-12.
  4. "Zanzibar International Film Festival (ZIFF)". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2014-08-11. Iliwekwa mnamo 2022-07-05.
  5. Public News Time (2022-06-03). "Zanzibar International Film Festival To Celebrate 25th Anniversary". Public News Time (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-19. Iliwekwa mnamo 2022-07-05.
  6. "Festival of the Dhow Countries Zanzibar International film festival | Safariland Cottages :: Arusha Hotel | Tanzania | Arusha Accommodation" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-19. Iliwekwa mnamo 2022-07-05.
  7. Pfaff, Françoise (2004). Focus on African films. Indiana University Press. uk. 277. ISBN 0-253-21668-0.
  8. "The European Day at the 25th Zanzibar International Film Festival | EEAS Website". www.eeas.europa.eu. Iliwekwa mnamo 2022-07-05.
  9. "Zanzibar festival aims to bridge ocean". BBC. 1999-07-06. Iliwekwa mnamo 2009-10-24.
  10. "Maangamizi Wins". GrisGrisFilms.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-27. Iliwekwa mnamo 2009-10-25. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  11. "Festival 2000 Awards Winner". Zanzibar.org. Iliwekwa mnamo 2009-10-25.
  12. "Golden Sandstorm Blows Over Zanzibar". FilmFestivals.com. 2001-07-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-07. Iliwekwa mnamo 2009-10-25. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  13. "Festival de Zanzibar : palmarès". Africultures.com. Julai 2005. Iliwekwa mnamo 2009-10-25.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. Lorey, Barbara (2006-09-08). "Setting Sail Over New Waters". Africultures.com. Iliwekwa mnamo 2009-10-25.
  15. "News & Events". Kenya Film Commission. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-25. Iliwekwa mnamo 2009-10-25. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  16. "Winning Films at ZIFF 2008". Official ZIFF website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 17, 2009. Iliwekwa mnamo 2009-10-25.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. "Zanzibar International Film Festival". Official ZIFF website. Iliwekwa mnamo 2009-10-25.
  18. "Zanzibar International Film Festival". Official ZIFF website. Iliwekwa mnamo 2010-07-19.
  19. 19.0 19.1 "Zanzibar International Film Festival". Official ZIFF website. Iliwekwa mnamo 2012-07-19.
  20. "Zanzibar International Film Festival". Official ZIFF website. Iliwekwa mnamo 2015-07-30.
  21. "Zanzibar International Film Festival". Official ZIFF website. Iliwekwa mnamo 2019-01-17.
  22. "Zanzibar International Film Festival". Official ZIFF website. Iliwekwa mnamo 2022-04-25.
  23. "ZIFF 2022 AWARDS | ZIFF 2022" (kwa American English). 2022-06-29. Iliwekwa mnamo 2022-07-05.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: