Teodoro wa Marseille

Teodoro wa Marseille (alifariki Marseille, Provence, leo nchini Ufaransa, 591) alikuwa askofu wa Marseille miaka 582-591. Alijitahidi kurudisha nidhamu katika Kanisa, na kwa ajili hiyo alihukumiwa na mfalme Kildebati na Gontran waliompeleka uhamishoni mara tatu[1].

Papa Gregori I alimuandikia barua ili asahihishe kosa la mapadri wake waliolazimisha Wayahudi kubatizwa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Januari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.