The Fox and the Hound
Makala hii au sehemu ya makala hii inahitaji masahihisho kwa upande mmoja wa zifuatazo:
|
The Fox and the Hound (kwa Kiswahili: Mbweha na Mbwa) ni filamu ya katuni iliyotolewa mwaka wa 1981. Filamu ilitayarishwa na Walt Disney Productions, na kutolewa kwenye kumbi za filamu tarehe 10 Julai 1981 na Buena Vista Distribution. Hii ni filamu ya ishirini na nne kutolewa katika mfululizo wa Walt Disney Animated Classics, na inatokana na kitabu cha Daniel P. Mannix chenye jina sawa na la filamu hii, na inahusu urafiki wa mbweha Tod na mbwa Copper.
The Fox and the Hound | |
---|---|
Posta ya filamu | |
Imeongozwa na | Ted Berman Richard Rich |
Imetayarishwa na | Ron Miller Art Stevens Wolfgang Reitherman |
Imetungwa na | Ted Berman Larry Clemmons |
Nyota | Mickey Rooney Kurt Russell Pearl Bailey Pat Buttram Sandy Duncan Richard Bakalyan Paul Winchell Jack Albertson Jeanette Nolan Keith Coogan Corey Feldman |
Muziki na | Buddy Baker |
Imesambazwa na | Buena Vista Distribution |
Imetolewa tar. | 10 Julai 1981 |
Ina muda wa dk. | Dk. 83 |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | $12 million[1] |
Mapato yote ya filamu | $39,900,000[2] |
Ikafuatiwa na | The Fox and the Hound 2 (2006) |
Nyota wa filamu hii waliotia sauti zao ni pamoja na Kurt Russell, Mickey Rooney, Pearl Bailey, Pat Buttram, Sandy Duncan, Richard Bakalyan, Paul Winchell, Jack Albertson, Jeanette Nolan, John Fiedler, John McIntire, Keith Mitchell, na Corey Feldman. Wakati wa kutolewa, ilikuwa ghali zaidi cartoon zinazozalishwa, kugharimu $12 milioni.[1] Ikafuatiwa na filamu, The Fox and the Hound 2, ilitolewa na DVD mnamo tarehe 12 Desemba 2006.
Hadithi
Filamu inaanza na mbwa mtoto ambaye ni yatima baada ya mama yake kuawa na wawindaji. Bundi mmoja anayejulikana kwa jina la Big Mama na ndege wawili ambao ni rafiki zake, sparrow aliyeitwa Dinky na kigong'ota aliyeitwa Boomer, wanapanga mpango wa yeye kulelewa na mjane mmoja aliyeitwa Widow Tweed. Mjane huyo akamwita mbwa jina la Tod, tangu hapo akawa anamkumbusha mara kwa mara juu ya kumfundisha kutembea mwenyewe.
Muda huohuo, jirani mmoja wa Tweed, mwindaji aliyejulikana kwa jina la Amos Slade, akamleta nyumbani mbweha mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Copper na kumtambulisha kwa mwimndaji mbwa wake mkuu aliyeitwa Chief. Tod na Copper wakawa marafiki, na kuapa kuwa watabaki kuwa "mrafiki milele."
Amos Slade akachukizwa na tabia ya Copper ya kwenda kucheza mara kwa mara, hivyo akaamua kumfungia. Wakati anacheza na Copper nyumbani kwake, Tod akamwamsha Chief. Slade na Chief wakamkimbiza hadi walipokuja kusimamishwa na Tweed.
Baada ya malumbano ya muda mrefu, Slade akasema kwamba anataka kumwua Tod na atafanya awezavyo ili ampate. Pale msimu wa uwindaji umefika akachukua mbwa zake na kuelekea kwenye safari yao ya uwindaji. Muda huohuo, Big Mama akamweleza Tod kwamba huu urafiki wake kati ya yeye na Copper hauwezi kuendelea tena, ikiwa wao ni maadui kiasili, lakini Tod hakutaka kumwani kabisa mama huyo.
Miezi ilipita, na Tod na Copper wamekuwa wakubwa sasa. Usiku mmoja wakati Copper anarudi, Tod akatokea na kumwuliza kama bado wangali marafiki. Copper akasema kwamba "siku hizo zishakwisha." na hivyo "Ninawinda mbwa sasa."
Copper akamwonya Tod kwamba Chief atamka, lakini Tod akasema kwamba Chief wala hanibabaishi. Chief akamka na kumwalifu Slade. Wakamkimbiza Tod na Copper. Copper akamwachia Tod aende zake na kuwaongoza Chief na Slade kwenda njia tofauti na ile alioenda nayo Tod, na Tod akajaribu kutoweka na gari moshi. Lakini kwa bahati mbaya Chief kambamba na kuanza kumtoa mbio Tod, halafu treni likaja na kumgonga Chief. Copper na Slade wakawa wanamlaumu Tod na kuapia kulipiza kisasi juu ya hilo.
Tweed akalijua kwamba Tod hayusalamani tena akiwa na yeye hivyo akafanya mchezo wa kumhifadhi. Big Mama akamtambulisha kwa mbweha mwanamke aliyeitwa Vixey, ambamo mambo yalionekana kuwa mazuri, lakini Slade na Copper wakavunja sehemu ile ya hifadhi na kuanza kuwawinda mbweha wawili.
Pale Slade yupo kwa kuwapiga, ghafula akatokea dubu mkubwa na kumshambulia. Akabululuka hadi na kujifunga kwenye mtego wake mwenyewe na kutupa silaha yake mbali kabisa na mahali alipo. Copper akaanza kupambana na dunu, lakini hakuwa sawa na yeye hivyo alishindwa. Tod akaanza kupambana na dubu hadi wote wakaanguka katika mapolomoko ya maji.
Copper akamtaka Tod ajifanye kama amelala chini ya ziwa hadi hapo Slade atapoonekana, akiwa tayari kufyatua mbweha. Copper akaingilia kati na kuziba na mwili wake ili Tod asipigwe, na kukataa kutoka. Mwishowe Slade akaamua kushusha silaha yake na kumwacha akiwa na Copper, lakini kama awali jinsi wawili hao walivyokuwa na ugomvi mkubwa. Leo hii wanashea na kufurahi pamoja baada ya kutengana.
Huko nyumbani, Tweed anamwuguza Slade arejee hali yake ya zamani wakati vijibwa vyake vimepumzika. Copper, kabla hajapumzika, akawa anatabasamu akikumbuka ile siku aliokuja kuwa rafiki na Tod. Kilimani anaonekana Vixey akiungana na Tod akiwa anatizama chini nyumbani kwa kina Copper na Tweed.
Washiriki
- Mickey Rooney kama Tod
- Kurt Russell kama Copper
- Pearl Bailey kama Big Mama
- Jack Albertson kama Amos Slade
- Jeanette Nolan kama Widow Tweed
- Pat Buttram kama Chief
- Keith Coogan kama Young Tod
- Corey Feldman kama Young Copper
- Sandy Duncan kama Vixey
- Paul Winchell kama Boomer
- Richard Bakalyan kama Dinkey
- John Fiedler kama Porcupine
- John McIntire kama Badger
Marejeo
- ↑ 1.0 1.1 Ansen, David (13 Julai 1981). "Forest Friendship". Newsweek: 81.
- ↑ "The Fox and the Hound (1981)". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2008-09-20.
Viungo vya nje
- (Kiingereza) The Fox and the Hound katika Allmovie
- The Fox and the Hound katika Internet Movie Database
- The Fox and the Hound katika Rotten Tomatoes