Theodoro Trikinas alikuwa mmonaki kutoka Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, katika karne ya 5.

Aliishi kiadilifu upwekeni katika monasteri ya Kalsedonia akijulikana kwa kuvaa kanzu moja tu za singa ndefu (ndiyo asili ya jina lake la pili) na kwa miujiza yake.[1][2]

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Aprili[3][4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.