Timbuktu (kifaransa: Tombouctou; kiarabu: تمبكتو) ni mji nchini Mali kusini ya jangwa la Sahara takriban kwa umbali wa 13 km na mto Niger. Leo kuna takriban wakazi 32,000 .

Msikiti ya kihistoria ya Djingerber

Kituo cha biashara ya Sahara

hariri

Timbuktu imejulikana zaidi kutokana na historia yake. Katika enzi ya kati mji ulikuwa kituo muhimu cha biashara ya misafara kupitia Sahara na pia kuvuka kanda la Sahel kusini ya jangwa hadi Sudan na Misri. Wakati ule mji uliunganishwa na mto Niger kwa mfereji ulioruhusu mashua ya biashara kufika sokoni moja kwa moja kutoka njia ya maji. Wakati ule mji ulikuwa na wakazi 100,000.

Utaalamu wa Kiislamu

hariri

Utajiri wa mji ulisaidia kujenga utamaduni wa kitaalamu. Kuna habari za madrasa 180 wakati moja. Hadi leo chuo kikuu cha Sankore ni dalili ya urithi huo kinaendelea kufanya kazi.

Baada ya kutekwa na Wamoroko mnamo 1591 Timbuktu haukustawi tena. Sababu muhimu pamoja na vita ni pia mabadiliko ya biashara; jahazi kwenye Atlantiki zilichukua sehemu kubwa ya biashara ya misafara kuvuka jangwani.

Timbuktu ilitembelewa mnamo mwaka 1510 na msafiri Mwarabu aliyejulikana baadaye kwa jina la Leo Africanus aliyepeleka habari za Timbuktu hadi Ulaya.

Timbuktu iliingizwa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO tangu 1988.

 
Geti ya kale ya Chuo Kikuu cha Sankore

Leo hii ni mji maskini unaotembelewa na watalii wachache wanaotafuta dalili za enzi za kale.

Tazama pia

hariri