Majengo
Majengo ni jina la mitaa mbalimbali katika miji ya Afrika ya Mashariki.
Kihistoria ilikuwa jina la makazi ya wafanyakazi Waafrika katika miji ya kikoloni. Ni kwamba Waingereza katika miji iliyoundwa nao katika Afrika ya Mashariki walifuata mpangilio uliokuwa na sehemu tatu[1]:
- Uzunguni kama sehemu ya nyumba za Wazungu na kando yake ofisi za serikali (mkuu wa wilaya, polisi, mahakama) [2]
- Uhindini [3] kama mtaa wa biashara iliyokuwa hasa mikononi mwa wafanyabiashara wenye asili ya Uhindi ya Kiingereza, katika miji mikubwa zaidi pia maduka ya Wazungu na
- Majengo[4] kama sehemu kwa wafanyakazi Waafrika na familia zao.
Katika miji mikubwa zaidi kulikuwa pia na sehemu ya pekee kwa wafanyakazi Wahindi wa matabaka ya chini[5]
Kata zinazoitwa "Majengo" zinapatikana katika wilaya za Tanzania kama ifuatavyo
- Majengo (Dodoma)
- Majengo (Kahama)
- Majengo (Kigoma)
- Majengo (Korogwe)
- Majengo (Lindi Vijijini)
- Majengo (Makambako)
- Majengo (Mbeya mjini)
- Majengo (Meru)
- Majengo (Monduli)
- Majengo (Moshi mjini)
- Majengo (Mpanda)
- Majengo (Mtwara Mjini)
- Majengo (Muheza)
- Majengo (Nkasi)
- Majengo (Singida)
- Majengo (Songea)
- Majengo (Sumbawanga mjini)
- Majengo (Tanga)
- Majengo (Tunduma)
- Majengo (Tunduru)
Pia kuna mitaa kama vile
Huko Kenya kuna
Marejeo
hariri- ↑ Kuhusu mpangilio wa miji katika Afrika ya Mashariki wakati wa ukoloni tazama Robert Home, Colonial Urban Planning in Anglophone Africa, uk. 60, ktk Carlos Nunes Silva (Ed.) (2015). Urban Planning in Sub-Saharan Africa: Colonial and Postcolonial Planning Cultures. New York, ISBN: 9780415632294
- ↑ "European residential"
- ↑ "Asiatic residential", katika miji midogo pamoja na "Commercial areas for Asiatics"
- ↑ "Native locations"
- ↑ "Locations for Asiatics of the working class"