Tombo
Tombo wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Galliformes (Ndege kama kuku)
Familia: Phasianidae (Ndege walio na mnasaba na kwale)
Jenasi: Anurophasis Oort, 1910

Coturnix Bonnaterre, 1791
Excalfactoria Linnaeus, 1766
Ophrysia Bonaparte, 1856
Perdicula Hodgson, 1837

Tombo (pia tomboo au tomboro) ni ndege wadogo wa jenasi kadhaa katika familia ya Phasianidae. Rangi yao ni kahawia na wana michirizi. Spishi nyingine zina rangi nyekundu na buluu. Kabla ya kuruka angani hungoja mpaka mtu ni karibu kuwakanyaga na huenda umbali fupi tu. Hula mbegu hasa lakini pengine hukamata wadudu pia. Hutaga mayai 6-18 ardhini.

Tombo wanatokea Afrika, Australasia na Ulaya. Kuna ndege huko Amerika ambao wana mnasaba na tombo, lakini wanaainishwa ndani ya familia Odontophoridae.

Spishi za AfrikaEdit

Spishi za mabara mengineEdit

PichaEdit