Chechele (Monarchidae)

(Elekezwa kutoka Trochocercus)
Chechele
Chechele wa Madagaska
Chechele wa Madagaska
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Monarchidae (Ndege walio na mnasaba na chechele)
Jenasi: Arses Lesson, 1831

Chasiempis Cabanis, 1847
Clytorhynchus Elliot, 1870
Eutrichomyias Meise, 1939
Hypothymis Boie, 1826
Mayrornis Wetmore, 1932
Metabolus Bonaparte, 1854
Monarcha Vigors & Horsfield, 1827
Myiagra Vigors & Horsfield, 1827
Neolalage Mathews, 1928
Pomaria Bonaparte, 1854
Terpsiphone Gloger, 1827
Trochocercus Cabanis, 1850

Spishi: Angalia katiba.

Chechele ni ndege wa familia Monarchidae. Kuna chechele wengine katika familia Stenostiridae. Zamani walikuwamo katika Monarchidae, lakini uchunguzi wa ADN unaonyesha kwamba hawana mnasaba na ndege hawa na wamepewa familia yao.

Chechele wa Monarchidae wana rangi kali, buluu na nyekundu hasa lakini njano pia; wengine ni weusi na weupe tu. Dume la spishi nyingi ana mkia mrefu sana. Wanatokea Afrika, Asia, Australia na visiwa vya Pasifiki. Spishi nyingi sana zinaishi msituni au katika maeneo yenye miti mingi, spishi chache katika savana kavu. Chechele hula wadudu ambao hukamata kama shore. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini. Mara nyingi huweka kuvumwani katika tago. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri