Tupac: Resurrection ilitolewa na Amaru Entertainment kama kibwagizo cha filamu ya makala kuhusu Tupac ya mwaka wa 2003. Tupac: Resurrection ilipata kuchaguliwa katika sherehe za Tuzo za Academy. Ina rekodi kadhaa zilizowahi kutolewa na 2Pac, ikiwa ni pamoja na "Death Around the Corner" kutoka katika Me Against the World, "Secretz of War" kutoka katika Still I Rise, Holler If Ya Hear Me kutoka katika Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z. na "Rebel of the Underground" kutoka katika 2Pacalypse Now; na mistari kadhaa ya 2Pac ambayo haikutolewa hapo awali na zimepangwa upya kwenye nyimbo mpya kama vile "Ghost", "One Day at a Time", na "Runnin (Dying to Live)".
Albamu imeenda kuuza nakala zaidi ya 420,000 na kupata hadhi ya platinum katika wiki yake ya kwanza. Eminem ametayarisha sehemu nyingi za albamu hii. Wimbo wa "Runnin (Dying to Live)" ulishinda tuzo ya Top Soundtrack Song of the Year kwenye sherehe za 2005 ASCAP Rhythm & Soul Music Awards. Albamu ina wasanii kama vile The Notorious B.I.G., Eminem, 50 Cent, Outlawz, na Digital Underground. "Intro", "Ghost", "Death Around The Corner", "Bury Me A G" and "Str8 Ballin'" hazikuwepo katika filamu hii, lakini zimeonekana katika albamu.
Imeuza nakala 1,666,335 huko nchini Marekani kwa mwaka wa 2011.[6]