Ujenzi mbunifu wa amani (sanaa)

Ujenzi wa amani bunifu (sanaa muonekano) hariri

ujenzi wa amani bunifu ni aina ya sanaa za kuona ambayo hutoa njia za kubuni ili kuleta amani katika miktadha yenye migogoro. Matumizi ya sanaa za kuona kwa ajili ya ujenzi wa amani kwa ufanisi unasisitiza kuzingatia asili ya muktadha ambapo zana inatumiwa bila kufuata mpangilio maalum au dhana. Inaonyesha uwezo wa kuvuka mawazo ya kimapokeo, kanuni, mifumo, mahusiano, na kadharika, ili kuunda mawazo mapya yenye mantiki, miundo, mbinu, na tafsiri zinazolenga kuanzisha na kudumisha amani. [1]

Kwa ujumla, sanaa ni nadharia na na muonekano halisi wa ubunifu unaopatikana katika jamii na tamaduni za watu. Aina kuu za sanaa ni pamoja na fasihi (mashairi, riwaya, hadithi fupi, na mashairi ya kishujaa), sanaa za maonyesho (muziki, kucheza, na maigizo), na sanaa za kuona, mwisho ni pamoja na ubunifu unaoweza kuonekana. Kulingana na kamusi ya Merriam-Webster, neno "ubunifu" hufafanua ubora wa kitu kilichoundwa badala ya kuigwa.[2] Hivyo, ujenzi wa amani bunifu ni neno pana la mikakati bunifu ya mahususi ili kuleta amani, baina ya watu binafsi, makundi, na jamii katika mazingira ya migogoro.[3]

Marejeo hariri

  1. "Creative Planning and Evaluating – Change Processes or Change Arts Projects?", Creative Partnerships in Practice : Developing Creative Learners (Bloomsbury Education), iliwekwa mnamo 2022-08-06 
  2. "Definition of Creative". Merriam-Webster. Retrieved 10 November 2017
  3. "Specific economic issues affecting peacebuilding in selected countries", Obstacles to Peacebuilding (Routledge), 2017-03-16: 117–147, ISBN 978-1-315-46641-5, iliwekwa mnamo 2022-08-06