Ukumbi (Kilolo)
Ukumbi ni kata ya Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51307.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 14,280 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,912 waishio humo.[2]
Kati ya vijiji vya kata hiyo, cha kwanza ni Kitowo. Kijiji cha Kitowo ni kijiji cha asili kilichopitiwa na barabara kuu ya mkoa wa Iringa kutoka Ihemi kupita Kitowo kwenda hospitali ya Usokami na Kihanzi, pacha nyingine kwenda Pomerini, Mgagao, Mtanga Farm n.k. na pacha nyingine kwenda Kilolo hadi Ipogolo.
Watu wa Kitowo ni wakulima wa:
- 1. mahindi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko vijiji vingine vyote vya wilaya ya Kilolo
- 2. nyanya, njegere na maharage
- 3. mboga za majani aina nyingi.
Historia ya uwanja wa ndege wa Nduli kwa Waingereza ina uhusiano mkubwa na kijiji cha Kitowo ambapo inaelezwa kuwa wakoloni walikuwa wanalima mali mbichi, hasa njegere Kitowo na kusafirisha hadi Dar es Salaam kupitia Nduli na wakoloni kula mboga asili za Kitowo. Meneja wa shamba hilo aliitwa Bwana Bodi na aliishi Ifuenga-Kitowo; ndiyo maana kuna njegere jina lake Bodi.
Marejeo
haririKata za Wilaya ya Kilolo - Tanzania | ||
---|---|---|
Boma la Ng'ombe | Dabaga | Ibumu | Idete | Ihimbo | Ilula | Image | Irole | Kimala | Kising'a | Lugalo | Mahenge | Masisiwe | Mlafu | Mtitu | Ng'ang'ange | Ng'uruhe | Nyalumbu | Nyanzwa | Ruaha Mbuyuni | Udekwa | Uhambingeto | Ukumbi | Ukwega |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ukumbi (Kilolo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |