Umimi ni tabia ya kujijali kupita kiasi, bila kutia maanani vya kutosha watu wengine na jamii kwa jumla.

Ni kinyume cha ukarimu na unamfanya mtu azingatie mno kinachompendeza au kinachomfaidisha yeye, badala ya kulenga pia kinachowafaa wengine.[1][2]

Umimi unatazamwa kwa namna mbalimbali na dini, falsafa, elimunafsia, uchumi na fani nyingine.

Katika Ugiriki ya KaleEdit

Aristotle aliungana na wananchi wenzake wengi katika kulaumu wanaolenga faida yao wenyewe tu.[3]

Seneca alipendekeza watu wajistawishe lakini ndani ya jamii.[4]

Karne za Kati/RenaissanceEdit

Ukristo wa Magharibi uliona umimi kama mzizi wa vilema vikuu vyote saba kwa jina la kiburi.[5]

Francis Bacon aliendeleza msimamo huo alipoandika, “Wisdom for a man's self...[a]s the wisdom of rats”.[6]

Ulimwengu wa kisasaEdit

Ubepari ulipoenea, Bernard Mandeville alisema maendeleo ya jamii na uchumi yanategemea umimi.[7]

Adam Smith alitumia mfano wa mkono usioonekana kusema mfumo wa uchumi unatumia umimi ili kuleta faida kubwa.[8]

Vilevile John Locke aliona jamii ijengwe juu ya mtu binafsi, halafu Ayn Rand alitetea umimi kama adili la kijamii ambalo ni mzizi wa maendeleo.[9]

Jacques Maritain alipinga hoja hizo kwa kukumbusha ile ya Aristotle kwamba binadamu ni kiumbe cha kijamii, hivyo anaweza kustawi kweli pande zote ikiwa tu analenga faida ya wengine.[10]

TanbihiEdit

  1. "Selfish", Merriam-Webster Dictionary, accessed on 23 August 2014
  2. Selfishness - meaning, reference.com, accessed on 23 April 2012
  3. Aristotle, Ethics (1976) p. 301-3
  4. G. Gutting ed., The Cambridge Companion to Foucault (2003) p. 138-30
  5. Dante, Purgatorio (1971) p. 65
  6. Francis Bacon, The Essays (1985) p. 131
  7. Mandeville, The Fable of the Bees (1970) p. 410 and p. 81-3
  8. M. Skousen, The Big Three in Economics (2007) p. 29
  9. P. L. Nevins, The Politics of Selfishness (2010) p. xii-iii
  10. Maritain, Jacques (1973). The Person and the Common Good. Notre Dame, IN: University of Notre Dame Press. ISBN 978-0268002046. 

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit