Shetani

Shetani (kwa Kiebrania שָׂטָן Satan, kwa Kigiriki Σατανᾶς Satanâs, kwa Kilatini Sátanas) ni jina linalomaanisha "Mpinzani"; "Mshtaki".

Shetani kadiri ya William Blake
Anguko la Shetani kadiri ya Gustave Doré

Kadiri ya imani ya dini mbalimbali, hasa zile zinazokubali ufunuo waliopewa Waisraeli, shetani ni malaika, roho, au mungu mdogo anayewakilisha uovu unaopingana na Mungu.

Shetani aajulikana pia kwa jina la Ibilisi (kutoka Kigiriki Diabolos, -ou, "Anayetenganisha"), Mtawala wa giza, Mkuu wa ulimwengu huu, Belzebub (jina la dhihaka kwa mungu Baal linalotafsiriwa "Bwana wa nzi"), Belial, Lusiferi (kutoka Kilatini Lucifer, "Mleta mwanga").

Baadhi ya watu, kwa mfano Wakristadelfiani, hufundisha kwamba Shetani ni mfano tu wa uovu na dhambi.

Marejeo