Waraka wa kwanza wa Yohane
Waraka wa kwanza wa Yohane ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Barua tatu za Yohane ziliandikwa kati ya mwaka 90 na 100 B.K., wakati ambapo jumuia za wafuasi wa Mtume Yohane zilianza kusambaratika.
Mafundisho na lugha vinalingana na vile vya Injili ya nne (Injili ya Yohane).
Barua ya tatu na ya pili hazina mafundisho muhimu, tofauti na ile ya kwanza inayodai imani sahihi na maisha matakatifu ili mtu astahili kuitwa Mkristo kweli.
Inakaza umwilisho wa Mwana wa Mungu na haja ya kuishi kwa uadilifu, na hasa kwa upendo (1Yoh 1:1-4; 2:3-11; 3:11-4:21; 2Yoh 7-13).
Marejeo
hariri- Robert Dabney, "The Doctrinal Various Readings of the New Testament Greek", 1894: p. 32.
Kiungo cha nje
hariri- [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa kwanza wa Yohane kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |