Unguja Ukuu ni eneo la kiakolojia kwenye kisiwa cha Unguja, takriban kilomita 25 kusini-mashariki mwa Jiji la Zanzibar, ndani ya kata ya Unguja Ukuu Kaepwani. Utafiti wa wanaakiolojia (Chittick 1966; Juma 2004) ulionyesha kwamba huko kulikuwa na kituo cha biashara ya kimataifa mnamo mwaka 800 BK.

Kati ya mabaki yaliyogunduliwa kuna vyungu kutoka Ghuba ya Uajemi, pamoja na vipande vya vyungu vya China na vilulu kutoka Sri Lanka[1]. Kuna pia mabaki ya jengo la mawe kutoka enzi ya mnamo mwaka 900 linaloaminiwa kuwa msikiti[2].

Tazama pia

Marejeo

  1. Mark Horton na Felix Chami: Swahili origins, uk. 141 katika "The Swahili World", Routledge 2018, ISBN: 978-1-138-91346-2
  2. Horton & Chami: Swahili origins, uk. 143 "A substantial stone building – possibly a mosque – was built at Unguja Ukuu at this time (Juma 2004). "

6°17′55″S 39°21′29″E / 6.2987°S 39.3580°E / -6.2987; 39.3580