Laurent Kabila

rais wa tatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Laurent-Désiré Kabila (27 Novemba 193918 Januari 2001) alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Mei 1997 hadi kuuawa 2001. Alifuatwa na mwanawe Joseph Kabila.

Kabila alifika ikulu kwa kumpindua Mobutu Sese Seko.

Asili ya KilubaEdit

Alizaliwa katika familia ya Waluba huko Baudouinville (sasa Moba) karibu na Albertville (Kalemie) kando la Ziwa Tanganyika. Alisoma huko Ujerumani ya Mashariki na Paris akarudi Kongo baada ya uhuru wa nchi alipojiunga na umoja wa vijana wa chama cha Patrice Lumumba.

Mwanaharakati wa LumumbaEdit

Baada ya kuuawa wa Lumumba alijiunga na kundi la wafuasi wa marehemu akaingia katika upinzani wa kijeshi dhidi ya serikali ya Joseph Desiree Mobutu. Majaribio haya yalikandamizwa na jeshi la serikali. Kabila alikuwa kati ya viongozi wachache walioendelea na upinzani.

Kiongozi wa vita ya msituniEdit

Alikuwa na usaidizi wa siri wa rais Julius Nyerere wa Tanzania na kwa miezi michache katika 1965 Mkuba Che Guevara alijiunga na kundi la Kabila lakini kufuatana na kumbukumbu za Guevara hawakuelewana wala kufanyikiwa.

Kuanzia 1967 aliungana na kundi dogo la Parti de la Revolution Populaire (PRP) akaongoza jeshi la Forces Armees Populaires (FAP) lililokuwa na makambi Tanzania na Zambia lakini aliweza pia kutawala eneo dodo katika milima ya Fizi ya mkoa wa Kivu hadi 1977 alipokufuzwa na jeshi la serikali ya Mobutu.

Baadaye aliishi Uganda na Tanzania hakuonekana tena Konfo. Hakushiriki katika uasi wa wanachi dhidi ya serikali ya Mobutu na jitihada ya kuongeza demokrasia nchini.

Kurudi kwa msaada wa RwandaEdit

Alirudi 1996 wakati wa uvamizi wa Kongo ya Mashariki ya wanamgambo Wahutu kutoka Rwanda. Mabaki ya jeshi la kihutu kutoka Rwanda walikuwa wamekimbilia Kongo 1994 baada ya mauaji ya kizazi ya Rwanda na sasa walishambulia Wabanyamulenge waliokuwa Watutsi wa Kongo. Serikali ya Rwanda ilitafuta njia ya kumaliza wanamgambo hao kwa sababu walikuwa tishio kwa utaratibu mpya wa Rwanda. Hapa walikuwa tayari kusaidia kujenga vikosi vya Wakongo wa kupambana na Wahutu katika Kongo.

Kabila aliunda maungano ya "Alliance des Forces Democratiques pour la Liberation du Congo-Zaire (AFDL)" akapokea silaha na washauri kutoka jeshi la Rwanda.

Katika muda mfupi Kabila aliweza kujipatia sifa kama kiongozi mwenye uwezo wa kushindana na jeshi la Mobutu aliyejua namna ya kufanya maazimio yake hata bila washauri wake Warwanda aliotegemea bado.

Mshindi dhidi ya MobutuEdit

Vikosi vya Kabila vilisogea mbele haraka dhidi ya jeshi la Mobutu isiyokuwa tayari tena ya kupigana na adui aliyejua kazi ya vita. Kabila alianza vita katika Oktoba 1996 huko Kivu akateka Bukavu Oktoba mwaka uleule, Kisangani katika Machi 1997 na Lumbumbashi mwezi wa Aprili. Mwezi wa Mei jeshi lake likaingia Kinshasa na wakubwa wa Mobutu walikimbia Brazzaville. Tar. 17 Mei Kabila alijitangaza kuwa rais mpya akabadilisha jina la nchi tena kuwa Kongo.

Kabila alikuwa na tatizo la kuwa hajakuwa na uhusiano wa watu wa Kinshasa ambao wengi walimwona kama mgeni. Askari zake wengi waliwasiliana kwa Kiswahili na Kiingereza au lugha za Kongo mashariki hawakujua Kifaransa wala lugha za Kongo magharibi. Baada ya kushika serikali Kabila alijaribu kupunguza umuhimu wa washauri wake Warwanda.

Rais wa kuona upinzaniEdit

Hii ilisababisha matatizo na uhusiano ulikuwa mbaya. Wananchi wa Kinshasa wengi hawakuona mabadiliko mengi katika maisha yao. Kabila hakuongeza haki za kidemokrasia wala kushirikiana na wanasiasa waliokuwa wapinzani wa kisiasa wa Mobutu katika miaka ya kutafuta demokrasia nchini.

Upinzani dhidi Kabila ikakua katika sehemu za nchi.

2001 aliuawa na askari wa ulinzi wake kwa namna isiyoeleweka vizuri hadi leo.

Wakuu wa jeshi walimtangaza mwana wake Joseph kuwa mfuasi wake.

Viungo vya NjeEdit