Uvimbe wa koromeo usababishwao na streptokoki

Uvimbe wa koromeo usababishwao na streptokoki (kwa Kiingereza Streptococcal pharyngitis au strep throat) ni ugonjwa ambao unasababishwa na bakteria inayoitwa “Streptococcus ya kundi A”.[1] Maambukizi yanaathiri koo na findo (tezi mbili katika koo nyuma ya mdomo). Maambukizi katika koo pia yanaweza kuathiri zoloto.

Streptococcal pharyngitis
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuOtolaryngology, infectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10J02.0
ICD-9034.0
DiseasesDB12507
MedlinePlus000639
eMedicinemed/1811

Dalili za kawaida ni pamoja na homa, uchungu kwa koo na tezi iliyofura (inayoitwa kivimbe timfu) katika shingo. Maambukizi katika koo inasababisha asilimia 37 ya uchungu wa koo miongoni mwa watoto.[2]

Maambukizi katika koo huenea kwa njia ya mawasiliano ya karibu na mgonjwa. Ili kuwa na uhakika mtu ana maambukizi katika koo, kipimo kinachoitwa throat culture kinahitajika. Hata bila kipimo hiki, ugonjwa huu unaweza kujulikana kwa sababu ya ishara.

Kiua vijasumu kinaweza kumsaidia mtu aliye na maambukizi katika koo. Kiuua vijasumu ni dawa ambazo huua bakteria. Hizo hutumika zaidi ili kuzuia matatizo kama vile homa kang’ata badala ya kufupisha urefu wa ugonjwa.[3]

Ishara na dalili

hariri

Dalili ya kawaida ni uchungu kwa koo, homa ya zaidi ya sentigredi 38°C (100.4°F), usaha (ugiligili wa manjano au kijani ulioundwa na bakteria waliokufa, na chembechembe nyeupe za damu) kwenye findo, na kivimbe timfu iliyofura.[3]

Kunaweza kuwa dalili nyingine kama vile:

Mtu ambaye amepatwa ataonyesha dalili siku moja hadi tatu baada ya kugusana na mtu mgonjwa.[3]

Chanzo

hariri

Maambukizi katika koo inasababishwa na aina ya bakteria inayoitwa kundi A beta-hemolytic streptococcus (GAS).[6]Bakteria au virusi vingine pia husababisha kuumwa na koo.[3][5] Watu hupata strep throat kwa mawasiliano ya moja kwa moja na mtu mgonjwa. Ugonjwa unaweza kuenea kwa urahisi zaidi wakati kuna umati wa watu.[5][7] Mifano ya umati ni pamoja na kwatu katika jeshi au katika shule.

Bakteria ya GAS inaweza kukauka katika vumbi, lakini haiwezi kufanya watu wawe wagonjwa. Kama bakteria yamewekwa katika mazingira ya unyevunyevu inaweza kufanya watu wawe wagonjwa hadi siku 15.[5] Bakteria nyevunyevu inaweza kupatikana kwenye vitu kama miswaki. Bakteria hawa wanaweza kuishi katika chakula, lakini hii si kawaida. Watu ambao wanakula chakula hicho wanaweza kugonjeka.[5] Asilimia kumi na mbili ya watoto wasiokuwa na ishara ya maambukizi katika koo wana GAS kawaida katika koo zao.[2]

Utambuzi wa ugonjwa

hariri
Alama Welekeo ya Kutibu Strep
1 au kidogo <Asilimia 10 Hakuna kiua vijasumu au uzoefu unahitajika
2 Asilimia 11–17 Inahusu kiua vijasumu kwenye uzoefu au RADT
3 Asilimia 28–35
4 au 5 Asilimia 52 Kiua vijasumu bila uzoefu

Orodha inayoitwa alama ya Kituo Kilichobadilishwa inasaidia madaktari kuamua jinsi ya kutunza watu walio na uchungu kooni. Alama ya kituo ina vipimo au uchunguzi tano za kliniki. Inaonyesha uwezekano wa jinsi vile mtu ana maambukizi katika koo.[3]

Hatua moja imetolewa kwa kila moja ya vigezo hivi:[3]

  • Hakuna kukohoa
  • Kivimbe timfu zilizofura au kivimbe timfu ambayo inauma ikiguswa
  • Halijoto kubwa kuliko sentigredi 38 (100.4°F)
  • Usaha au kufura kwa findo
  • Chini ya umri wa miaka 15 (sehemu huchukuliwa kama mtu ana zaidi ya miaka 44)

Uchunguzi wa maabara

hariri

Jaribio linaloitwa throat culture ni njia kuu[8] ya kujua kama mtu anayo maambukizi katika koo. Kipimo hiki ni sahihi kwa asilimia 90 hadi 95.[3]

Kuna kipimo kingine kinachoitwa rapid strep test, au RADT. Hiyo ni ya haraka kuliko throat culture lakini kwa usahihi inapata ugonjwa kwa asilimia 70.

Vipimo vyote huonyesha wakati mtu hana strep throat. Wanaweza kuonyesha hili kwa usahihi kwa asilimia 98 ya muda. [3]

Wakati mtu ni mgonjwa kipimo cha throat culture au rapid strep inaweza kubaini kama mtu ni mgonjwa kutokana na strep throat.[9] Watu ambao hawana dalili wanapaswa wapimwe kipimo cha throat culture au rapid strep kwani baadhi ya watu wana bakteria ya streptococcal katika koo zao kwa kawaida bila ya matokeo yoyote mabaya. Na watu hawa hawahitaji matibabu. [9]

Vyanzo vya dalili sawa

hariri

Strep throat ina baadhi ya dalili sawa kama magonjwa mengine. Kwa sababu ya haya, inaweza kuwa vigumu kujua kama mtu ana strep throat bila ya kipimo cha throat culture au rapid throat test.[3] Kama mtu ana homa na uchungu kwa koo na kukohoa, mafua, kuhara, na hisia ya macho mekundu yanayowasha, huenda ikawa ni uchungu wa koo ambayo inasababishwa na virusi.[3] Maambukizi mononucleosis inaweza kusababisha kivimbe timfu iliyovimba katika shingo na koo, homa, na inaweza kufanya findo kuwa kubwa.[10] Utambuzi huu unaweza kuamuliwa na uchunguzi wa damu. Hatahivyo hakuna tiba maalum kwa ajili ya kuambukiza ya mononucleosis.

Baadhi ya watu hupata strep throat mara nyingi kuliko wengine. Kuondoa findo ni njia moja ya kuzuia watu hawa kutopata strep throat tena.[11][12] Kupata strep throat mara tatu au zaidi kwa mwaka moja inaweza kuwa sababu nzuri ya kuondoa findo.[13] Kusubiri pia ni sahihi.[11]

Matibabu

hariri

Maambukizi katika koo kwa kawaida huchukua muda wa siku chache bila matibabu.[3] Kutibu na kiua vijasumu kwa kawaida hufanya dalili kupotea masaa 16 kwa haraka. [3] Sababu kubwa kwa ajili ya kutibu na kiua vimelea ni kupunguza hatari ya kupata ugonjwa mbaya zaidi. Kwa mfano, ugonjwa wa moyo unaojulikana kama homa kang’ata au ukusanyaji wa usaha katika koo inajulikana kama retropharyngeal abscess.[3] Kiua vijasumu kitafanya kazi vizuri kikitolewa ndani ya siku 9 za mwanzo wa dalili.[6]

Dawa ya maumivu

hariri

Dawa ya kupunguza maumivu inaweza kusaidia uchungu unaosababishwa na strep throat.[14] Kwa kawaida hizi ni pamoja na NSAID aur paracetamol ambayo pia inajulikana kama acetaminophen. Steroidi pia ni muhimu[6], kama ulimo lidocaine.[15] Aspirini inaweza kutumiwa kwa watu wazima. Si vizuri kuwapa watoto aspirini kwa sababu inawafanya kuwa na uwezekano wa kupata Ugonjwa wa Reye.[6]

Dawa ya kiua vijasumu

hariri

Penicillin V ni kiua vijasumu ya kawaida inayotumika nchini Marekani kwa maambukizi katika koo. Ni maarufu kwa sababu ni salama, inafanya kazi vizuri na haigharimu pesa pesa nyingi.[3] Amoxicillin kwa kawaida hutumika barani Uropa.[16] Nchini India sanasana ni ya watu wanaopata homa ya yabisi. Kwa sababu hiyo, dawa ya kudunga inayoitwa benzathine penicillin G ni tiba ya kawaida.[6] Kiua vijasumu hupunguza urefu wa wastani ya dalili. Urefu wa wastani siku tatu hadi tano. Kiua vijasumu inapunguza hii kwa siku moja. Dawa hizi pia kupunguza maambukizi ya ugonjwa.[9] Dawa hutumika zaidi na inajaribu kupunguza matatizo kwa nadra. Hizi ni pamoja na homa kang’ata, upele au maambukizi.[17] Madhara mazuri ya kiua vijasumu inapaswa iwe na uwiano na uwezekano wa athari zake. [5] Matibabu ya kiua vijasumu haihitaji kupewa kwa watu wazima walio na afya ambao wamekuwa na athari mbaya kwa dawa. [17] Kiua vijasumu hutumiwa kwa ajili ya strep throat mara nyingi zaidi kuliko inavyotarajiwa kutoka jinsi ilivyo kali na kwa kasi ambavyo huenea.[18]Dawa erythromycin (na dawa zingine, zinazoitwamacrolide) zinapaswa zitumike kwa watu ambao wana mizio mbaya kwa penicillin.[3]Cephalosporin inaweza kutumiwa kwa watu walio na mzio kidogo.[3] Maambukizi ya Streptococcal pia inaweza kusababisha uvimbe wa figo (glomerulonephritis kali). Kiua vijasumu haipunguzi uwezekano wa hali hii. [6]

Mtazamo

hariri

Dalili za maambukizi katika koo kawaida hupata kuwa bora, na au bila ya tiba, katika muda wa siku tatu hadi tano.[9]Matibabu na viua vijasumu hupunguza hatari ya magonjwa mabaya zaidi. Pia huifanya vigumu kueneza ugonjwa. Watoto wanaweza kurejea shuleni masaa 24 baada ya kuchukua kiua vijasumu.[3]

Matatizo haya mabaya sana inaweza kusababishwa na maambukizi katika koo:

Uwezekano

hariri

Strep throat ni pamoja na kundi pana la uchungu wa koo au uvimbe wa koromeo. Kadiri ya watu milioni 11 hupata kidonda kooni nchini Marekani kila mwaka.[3] Kesi nyingi za vidonda vya koo husababishwa na virusi. Bakteria Kundi A Streptokokasi beta-hemolytic husababisha asilimia 15-30 ya vidonda vya kooni kwa watoto. Husababisha asilimia 5 hadi 20 ya vidonda vya kooni kwa watu wazima.[3] Kesi kwa kawaida hutokea katika majira ya baridi na mapema katika majira ya kuchipua.[3]

Marejeo

hariri
  1. "streptococcal pharyngitis" at Dorland's Medical Dictionary
  2. 2.0 2.1 Shaikh N, Leonard E, Martin JM (2010). "Prevalence of streptococcal pharyngitis and streptococcal carriage in children: a meta-analysis". Pediatrics. 126 (3): e557–64. doi:10.1542/peds.2009-2648. PMID 20696723. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 3.13 3.14 3.15 3.16 3.17 3.18 3.19 3.20 3.21 Choby BA (2009). "Diagnosis and treatment of streptococcal pharyngitis". Am Fam Physician. 79 (5): 383–90. PMID 19275067. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Brook I, Dohar JE (2006). "Management of group A beta-hemolytic streptococcal pharyngotonsillitis in children". J Fam Pract. 55 (12): S1–11, quiz S12. PMID 17137534. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 Hayes CS, Williamson H (2001). "Management of Group A beta-hemolytic streptococcal pharyngitis". Am Fam Physician. 63 (8): 1557–64. PMID 11327431. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-16. Iliwekwa mnamo 2012-05-08. {{cite journal}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |month= ignored (help)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 6.5 Baltimore RS (2010). "Re-evaluation of antibiotic treatment of streptococcal pharyngitis". Curr. Opin. Pediatr. 22 (1): 77–82. doi:10.1097/MOP.0b013e32833502e7. PMID 19996970. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  7. Lindbaek M, Høiby EA, Lermark G, Steinsholt IM, Hjortdahl P (2004). "Predictors for spread of clinical group A streptococcal tonsillitis within the household". Scand J Prim Health Care. 22 (4): 239–43. doi:10.1080/02813430410006729. PMID 15765640.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  8. Smith, Ellen Reid; Kahan, Scott; Miller, Redonda G. (2008). In A Page Signs & Symptoms. In a Page Series. Hagerstown, Maryland: Lippincott Williams & Wilkins. uk. 312. ISBN 0-7817-7043-2.
  9. 9.0 9.1 9.2 9.3 Bisno AL, Gerber MA, Gwaltney JM, Kaplan EL, Schwartz RH; Gwaltney (2002). Clin. Infect. Dis. 35 (2): 113–25. doi:10.1086/340949. PMID 12087516. {{cite journal}}: Missing |author2= (help); Missing or empty |title= (help); Unknown parameter |Kichwa= ignored (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  10. Ebell MH (2004). "Epstein-Barr virus infectious mononucleosis". Am Fam Physician. 70 (7): 1279–87. PMID 15508538. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-24. Iliwekwa mnamo 2012-05-08. {{cite journal}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  11. 11.0 11.1 Paradise JL, Bluestone CD, Bachman RZ; na wenz. (1984). "Efficacy of tonsillectomy for recurrent throat infection in severely affected children. Results of parallel randomized and nonrandomized clinical trials". N. Engl. J. Med. 310 (11): 674–83. doi:10.1056/NEJM198403153101102. PMID 6700642. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  12. Alho OP, Koivunen P, Penna T, Teppo H, Koskela M, Luotonen J (2007). "Tonsillectomy versus watchful waiting in recurrent streptococcal pharyngitis in adults: randomised controlled trial". BMJ. 334 (7600): 939. doi:10.1136/bmj.39140.632604.55. PMC 1865439. PMID 17347187. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  13. Johnson BC, Alvi A (2003). "Cost-effective workup for tonsillitis. Testing, treatment, and potential complications". Postgrad Med. 113 (3): 115–8, 121. PMID 12647478. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  14. Thomas M, Del Mar C, Glasziou P (2000). "How effective are treatments other than antibiotics for acute sore throat?". Br J Gen Pract. 50 (459): 817–20. PMC 1313826. PMID 11127175. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  15. "Generic Name: Lidocaine Viscous (Xylocaine Viscous) side effects, medical uses, and drug interactions". MedicineNet.com. Iliwekwa mnamo 2010-05-07.
  16. Bonsignori F, Chiappini E, De Martino M (2010). "The infections of the upper respiratory tract in children". Int J Immunopathol Pharmacol. 23 (1 Suppl): 16–9. PMID 20152073.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  17. 17.0 17.1 Snow V, Mottur-Pilson C, Cooper RJ, Hoffman JR (2001). "Principles of appropriate antibiotic use for acute pharyngitis in adults" (PDF). Ann Intern Med. 134 (6): 506–8. PMID 11255529. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  18. Linder JA, Bates DW, Lee GM, Finkelstein JA (2005). "Antibiotic treatment of children with sore throat". J Am Med Assoc. 294 (18): 2315–22. doi:10.1001/jama.294.18.2315. PMID 16278359. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  19. 19.0 19.1 "UpToDate Inc". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-08. {{cite web}}: Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20081208133138/http://www.utdol.com/online/content/topic.do?topicKey= ignored (help)
  20. Stevens DL, Tanner MH, Winship J; na wenz. (1989). "Severe group A streptococcal infections associated with a toxic shock-like syndrome and scarlet fever toxin A". N. Engl. J. Med. 321 (1): 1–7. doi:10.1056/NEJM198907063210101. PMID 2659990. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  21. 21.0 21.1 Hahn RG, Knox LM, Forman TA (2005). "Evaluation of poststreptococcal illness". Am Fam Physician. 71 (10): 1949–54. PMID 15926411. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)