Uzamivu

(Elekezwa kutoka Uzamifu)

Uzamivu (pia PhD ambayo ni kifupi cha Kilatini "Philosophiae Doctor" yaani "Daktari wa Falsafa") ni shahada ya juu kabisa katika elimu.

Muhitimu wa ngazi ya PHD huko Afrika ya Kusini akiwa katika vazi maalumu

Inatolewa na vyuo vikuu baada ya digrii ya kwanza na shahada ya uzamili.

Kwa kufuata tabia za lugha nyingine, jina daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uzamivu. Katika nchi nyingi, mtu aliyepokea shahada ya uzamivu anaongeza cheo kabla ya jina lake kwa kifupi ambacho kimatifa ni "Dr.", kwa Kiswahili mara nyingi pia "Dkt."

Ilikuwa desturi hadi leo kwamba mgombea wa uzamivu anaonyesha uwezo wake kwa kutunga tasnifu ambayo ni kitabu kamili. Siku hizi masharti ya tasnifu yanaweza kutimizwa pia kwa kutunga idadi fulani za makala zinazohitaji kupokewa na majarida ya kitaalamu ambamo zinachunguliwa na wataalamu wengine kabla ya kupokewa na kuchapishwa.

Nje ya utaratibu wa kawaida kuna pia cheo cha "daktari wa heshima" hutolewa kwa mtu anayetazamiwa kuwa na michango mikubwa kwa maendeleo ya sayansi fulani, elimu kwa jumla au kwa taasisi ya elimu. Mara nyingi hutolewa pia kwa sababu za kisiasa. Kifupi chake kwa kawaida ni "Dr. h.c."; "h.c." ni kifupi cha Kilatini honoris causa kinachomaanisha "kwa sababu ya heshima".

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uzamivu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.