Valeriano wa Avensano

Valeriano wa Avensano (377 hivi - 457) alikuwa askofu wa Avensa, leo Bordj-Hamdouna, Tunisia, katika karne ya 5, ambaye pamoja na maaskofu wenzake 8 alifukuzwa mjini na mfalme Genseriki wa Wavandali kwa amri ya kwamba mtu yeyote asimkaribishe nyumbani wala shambani kwa sababu alikataa katakata kukabidhi vifaa vya ibada.

Kwa hiyo alilala muda mrefu barabarani ingawa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 80 [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 15 Desemba[2], lakini pia 28 Novemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.