Veneri wa Milano (kwa Kilatini: Venerius; alifariki Milano, Italia, 408 hivi) alikuwa Askofu wa mji huo tangu mwaka 400 (au 401) hadi kifo chake.

Mt. Veneri wa Milano

Alipokuwa shemasi wa Ambrosi wa Milano, alihudhuria kifo chake.

Kama askofu alituma wakleri kusaidia Kanisa la Afrika Kaskazini, mmojawao akiwa mwanahistoria Paulino Shemasi aliyeandika habari zake.

Pia alimtetea na kumtunza Yohane Krisostomo alipokuwa uhamishoni[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Mei[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.