Verdiana Masanja

mwanahisabati wa kike Tanzania


Verdiana Grace Masanja (alizaliwa mjini Bukoba, nchini Tanzania, 12 Oktoba 1954)[1] ni mwanahisabati na mwanamke wa kwanza Mtanzania kupata shahada ya uzamivu katika Hisabati.

Verdiana Masanja
Amezaliwa12 Oktoba 1954
UtaifaMtanzania
Majina mengineVerdiana Grace Kashaga
Kazi yakeMhadhiri na Profesa wa Hisabati

Tangu mwaka 2018 ni profesa wa hisabati kwenye Taasisi ya Kiafrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela huko Arusha, Tanzania.

Profesa Masanja pia anajulikana kwa kushiriki katika kuinua wanawake na elimu kwa wanawake.

Maisha ya awaliEdit

Masanja alizaliwa kwenye familia ya Kashaga mjini Bukoba, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania karibuni na mpakani na Uganda. Wakati huo, Tanzania bara iliitwa Tanganyika na ilitawaliwa na wakoloni wa Uingereza [2][3].

ElimuEdit

Masanja alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Nyakabungo jijini Mwanza. Aliendelea na elimu ya sekondari kwenye shule za sekondari za Chopre (kwa sasa Mwanza) na Rosary (kwa sasa Ngaza), zote zikiwemo jijini Mwanza[4]. Anasemekana kuongoza kwa ufaulu darasani, na alipewa jina la Imani "jike dume". Alipata elimu ya sekondari ya juu Jangwani High School mjini Dar es Salaam. Baada ya hapa, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa jailli ya Massomo ya shahada ya kwanza ya hisabati na fizikia ambapo alimaliza mwaka 1976. Aliendelea na masomo ya shahada ya uzamili aliyoipata mnamo mwaka 1981 kwenye Chuo hicho hicho. Tasnifu ya shada ya uzamili iliandikwa chini ya Kichwa Effect of Injection on Developing Laminar Flow of Reiner-Philippoff Fluids in a Circular Pipe[5].

 
Prof. Verediana Masanja Akielekezwa jambo wakati wa Warsha ya Astronomia


Baada ya shahada ya uzamili, aliendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Ufundi Berlin, Ujerumani (wakati huo Ujerumani Magharibi), ambapo alipokea shahada ya uzamivu mnamo mwaka wa 1986 na kuandika tasnifu yenye kichwa A numerical study of a Reiner-Rivlin Fluid in an axi-symmetrical circular pipe[6].

KaziEdit

Masanja aliajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza shahada ya uzamivu nchini Ujerumani. Alifundisha kozi za hesabu kwa wanafunzi wa shahada ka kwanza, uzamivu na uzamili. Pia alisimamia wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu kwenye tafiti na tasnifu zao[7]. Aliwahi kuongoza idara ya hisabati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1994 hadi 2000 [8]. Alibakia kua mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi maka 2010.

Tangu mwaka 2006 alifundisha Chuo Kikuu cha Rwanda ambapo mwaka 2007 aliteuliwa kua mkurugenzi wa utafiti. Baadae aliteuliwa kua naibu kansela na mshauri mwandamizi juu ya mikakati-maendeleo, utafiti na uvumbuzi kwenye Chuo Kikuu cha Kibungo, nchini Rwanda[9][10].

Mwaka 2018, alichukua nafasi kama profesa kamili wa hisabati tumizi na matumizi ya kompyuta katika Taasisi ya Kiafrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela[11].

Nje ya Kazi, Masanja alijishughulisha katika kuhakikisha anawawezesha katika elimu ya hisabati na sayansi wasichana na wanawake nchini Tanzania na katika Afrika kwa jumla.

Kujihusisha na Miradi ya KielimuEdit

Aliwahi kushiriki warsha ya Astronomia akiwa kama muelimishaji wa maswala mbalimbali.

MarejeoEdit

 1. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020
 2. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020
 3. African Doctorates in Mathematics: A Catalogue, uk. 718, iliangaliwa kupitia google books tar. 1. Desemba 2018
 4. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020
 5. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020
 6. Verdiana Grace Masanja kwenye tovuti ya Mathematics Genealogy Project ya North Dakota State University, Marekani, iliangaliwa Desemba 2018
 7. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020
 8. L.H. Riddle, makala "Verdiana Grace Masanja" katika Biographies of Women Mathematicians, kwenye tovuti ya Agnes Scott College, Memphis, Marekani
 9. Ms Verdiana Grace Masanja, tovuti ya net4mobility.eu ya mradi wa Horizon 2020 ya Umoja wa Ulaya
 10. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020
 11. http://mathshistory.st-andrews.ac.uk/Biographies/Masanja.html, iliangaliwa tar. 9 April 2020

Viungo vya NjeEdit

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Verdiana Masanja kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.