Verena wa Zurzach
Verena wa Zurzach (Garagos, karibu na Thebe, leo Luxor, Misri, 260 hivi – Bad Zurzach, Uswisi, 14 Septemba 344) alikuwa msichana aliyelelewa Kikristo na familia yake na hatimaye alibatizwa.
Alifuatana na ndugu yake askari wa Kikosi cha Thebe hadi Uswisi alipoishi kwanza kama mkaapweke halafu akawa anasaidia wengi[1][2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu[4].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba[5].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Our Patron: Saint Verena", Santa Verena Charity
- ↑ Monks of Ramsgate. “Verena”. Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 1 September 2016
- ↑ "Coptic Saint Verena, the Egyptian who taught Europe personal hygiene, Al Arabiya, 10 April 2017
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/91316
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |