Victoria Beckham
Victoria Caroline Beckham (amezaliwa 17 Aprili 1974) ni mwimbaji na msanifu mavazi kutoka nchini Uingereza. Anafahamika sana kwa kuwa mmoja kati ya wanakundi la wasichana waimbao muziki wa pop la Spice Girls. Pia, anafahamika zaidi kwa vile kaolewa na mchezaji mashuhuri wa soka ya kulipwa huko Uingereza - David Beckham.
Victoria Beckham | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Victoria Caroline Adams |
Amezaliwa | 17 Aprili 1974 Goffs Oak, Hertfordshire, Uingereza |
Aina ya muziki | Pop |
Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, msanifu wa mavazi, mfanyabiashara |
Miaka ya kazi | 1994-mpaka sasa |
Studio | Virgin, 19, Telstar |
Ame/Wameshirikiana na | Spice Girls |
Jina lake la utani ni Posh Spice, kwa sababu anapenda kuvaa nguo zinazompendezesha.
Viungo vya nje
hariri- Victoria Beckham's official site Ilihifadhiwa 30 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Victoria Beckham Collection website Ilihifadhiwa 28 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Victoria Beckham at the Internet Movie Database
Makala hii kuhusu mwanamuziki wa Uingereza bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Victoria Beckham kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |