Viongozi wa Hezbollah waliouawa na Israeli

Viongozi wa Hezbollah waliouawa na Israeli mwaka 2024 wamefikia saba. Makamanda hao waliouawa kisiasa kupitia mashambulizi ya anga ya Israeli ni pamoja na Kiongozi Mkuu wa kundi hilo la kijeshi, Hassan Nasrallah ambaye alipouawa alikuwa kwenye makao makuu yake yaliyojengwa ardhini huko Beirut.[1]

ndege ya Jeshi la Anga la Israeli F-15I iliyobeba mabomu yaliyoboreshewa ulengaji shabaha ikipaa kwenda kushambulia mnamo Sept. 27,2024

Mashambulizi hayo yaliyofanywa na Israeli yanaipa Hezbollah, kundi linalofadhiliwa na Iran, pigo kubwa kuliko lolote lililowahi kulipata tangu liasisiwe mwaka 1982.

Orodha yao na udadavuzi mfupi

hariri

Fu'ad Shukr (Aliuawa Julai 30, 2024)

 
Fuad_shukr

Alikuwa ni mmoja wa makamanda waandamizi wa Hezbollah na mjumbe wa Baraza la Jihad. Fuad alitazamwa kama mrithi wa baadae wa Hassan Nasrallah. Kabla ya kuuawa, serikali ya Marekani ilitangaza dau la dola milioni tano kwa yeyote ambaye angetoa taarifa za kuwezesha kukamatwa kwake. Aliuawa Kwa shambulio la droni (ndege isiyo na rubani) kwenye viunga vya jiji la Beirut.[2]

Ibrahim Aqil (Aliuawa Sept. 20, 2024)

 
Ibrahim Aqil

Aqil alikuwa Kamanda Mkuu na muasisi wa Jeshi la Kisomi la Radwan la Hezbollah. Serikali ya Marekani ilimwekea dau la dola milioni saba mtu ambaye angewezesha kupatikana kwake sababu ikiwa ni kushukiwa kwake kuhusika na tukio la kuulipua ubalozi wa Marekani huko Beirut, Lebanon, mwaka 1983 na ulipuaji wa kambi za wanajeshi wanamaji wa jiji hilo. Aliuawa akiwa na makamanda wengine kwenye jengo moja maeneo ya Dahiyeh karibu na Beirut.[3]

Ahmad Wehbe (Aliuawa Sept. 20, 2024) Alikuwa kamanda mwandamizi wa Jeshi la Radwan la Hezbollah. Aliuawa pamoja na Aqil wilayani Dehiyeh.

Ibrahim Kobeissi (Aliuawa Sept. 25, 2024) Alikuwa kamanda wa kitengo cha makombora cha Hezbollah. Aliuawa kwa kombora kwenye viunga vya kusini mwa jiji la Beirut.[4]

Mohammad Surour (Aliuawa Sept. 26, 2024) Surour alikuwa mkuu wa kitengo kipya cha droni cha Hezbollah na ndiye aliyepanga mashambulizi ya makombora dhidi ya Israeli kutokea Lebanon. Aliuawa kwa shambulio la anga akiwa Beirut.[5]

Hassan Nasrallah (Aliuawa Sept. 27, 2024)

 
Sayyid Hassan Nasrallah

Nasrallah alichukua uongozi wa Hezbollah mnamo mwaka 1992 baada ya mtangulizi wake Abbas al-Musawi kuuawa kisiasa kwa shambulio la helikopta ya Israeli. Yeye ndiye aliyetengeneza mageuzi makubwa ya chama chake na kuwa ni nguzo yenye nguvu kwenye siasa za Lebanoni. Aliuawa kwa shambulio la Israeli akiwa ndani ya makao makuu yake yaliyokuwa ya chini kwa chini kusini mwa Beirut, pamoja na maafisa wengine 20.[6]

Nabil Qaouk (Aliuawa Sept. 29, 2024)

 
Sheikh Nabil Qaouk

Alikuwa kamanda wa Hezbollah wa kitengo cha kujihami kiusalama na mjumbe wa Baraza Kuu la Hezbollah. Marekani ilimtaja kama gaidi wa kimataifa mnamo Oktoba 2020 na akawekewa vikwazo. Aliuawa na shambulio la Israeli kwenye eneo la mbali na Beirut la Chyah.[7]

Tanbihi

hariri