Vita ya Kijerumani

Vita ya Kijerumani ya 1866 (inaitwa pia Vita ya Austria dhidi ya Prussia, au Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Ujerumani; kwa Kijer.: Deutscher Krieg) ilipiganwa mnamo 1866 kati ya Milki ya Austria kama kiongozi wa Shirikisho la Ujerumani na Ufalme wa Prussia. Prussia ilisaidiwa hasa na Italia pamoja na madola madogo ndani ya Ujerumani.

Ramani ya Ujerumani wakati wa vita ya 1866; nyekundu: Austria; nyekundu nyeupe: Madola ya Shirikisho la Ujerumani yaliyoshikamana na Austria; buluu: Prussia; buluu nyeupe: Madola ya Ujerumani yaliyoshikamana na Prussia

Vita hiyo ilikuwa sehemu ya mwisho ya ushindani kati ya Austria na Prussia kuhusu kipaumbele katika Ujerumani kwa jumla. Tokeo lake lilikuwa ushindi wa Prussia, kuondoka kwa Austria katika siasa ya Ujerumani na ukuu wa Prussia juu ya madola mengine ya Ujerumani.

Prussia ilifaulu kushinda majeshi ya Hannover na Bavaria pekepeke kabla hayajafaulu kuungana. Kwenye mapigano ya Koeniggraetz ilishinda pia jeshi kuu la Austria.[1]

Vita ilimaliza Shirikisho la Ujerumani lililoondolewa. Prussia haikudai maeneo ya Austria lakini ilimeza madola ya Ufalme wa Hannover na temi za Hessen zilizoendelea kama mikoa ya Prussia[2]. Sehemu za kaskazini za Ujerumani ziliungana katika Shirikisho la Ujerumani Kaskazini chini ya uongozi wa Prussia.

Italia iliwahi kushambulia Milki ya Austria katika majimbo yake kaskazini mwa rasi ya Italia; inagawa jeshi lake halikufaulu katika mashambulio yake, baada ya vita Austria ilipaswa kukabidhi maeneo ya Venezia na Mantova kwa Ufalme wa Italia.

Marejeo

hariri
  1. The campaign of 1866 in Germany, by col. von Wright and capt. H.M. Hozier, uk 362
  2. Schmitt, Hans A. (1975). "Prussia's Last Fling: The Annexation of Hanover, Hesse, Frankfurt, and Nassau, June 15 -October 8, 1866". Central European History. 8 (4): 316–347. doi:10.1017/S0008938900018008. S2CID 145525529
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Kijerumani kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.