Wadorobo
Wadorobo au Wandorobo ni wawindaji-wakusanyaji wenye asili ya kuishi porini nchini Kenya na Tanzania. Jina hilo linatokana na Kimasai likimaanisha "wawindaji", yaani watu wanaoishi bila kumiliki mifugo. Wengi wao wanaishi kwa kushirikiana na Wamasai kama tabaka la chini.
Chakula chao asili ni asali pamoja na nyama.
Hao ni watu wenye kupenda utamaduni kwelikweli, pia ni watu wenye matambiko; kama una tatizo ukiwaita wanakutambikia. Katika mila zao kuna mambo ambayo huwezi kuyafahamu mpaka "ufumbaswe": neno hili lina maana kwamba wanaofumbaswa ni watoto wa kiume tu na huwezi kwenda kwenye mizimu kama hujafumbaswa, usije ukapata matatizo kama upele, upofu n.k. Vitu vinavyotakiwa ili kufumbaswa ni asali, halafu inapikwa pombe mitungi saba: hapo kuna mtungi wa baba mtu, mjomba, mama, bibi, babu, shangazi n.k.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wadorobo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wadorobo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |