Wafiadini wa Mlima Sinai
Wafiadini wa Mlima Sinai (waliishi karne ya 4) ni wamonaki Wakristo 38 wa Misri waliouawa huko na Wablemi, kadiri ya simulizi la Nilo wa Sinai, wakiwemo Isaya, Jesaja, Saba, Musa, Musa mwingine, Yeremia, Paulo, Adamu, Serjio, Domnus, Proklo, Ipasi, Isaka, Makari, Marko, Benyamini, Eusebi, Elia na Theodulo [1][2][3].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 14 Januari[4].
Pengine wanachanganywa na wamonaki 43 waliouawa Raithu, karibu na mlima Sinai, hapo baadaye (karne ya 5) na walioandikiwa na Amoni fulani [5]. Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 22 Desemba[6].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |