Wasweta ni kabila dogo la jamii ya Wakurya. Wanaishi mkoani Mara Wilayani Rorya katika vijiji vya Kyangasaga, Isegere, Gabimori na Sonjo ndani ya kata ya Kyangasaga; pia wanapatikana Kibuyi.

Kwa kuwa wanaishi kando ya ziwa Viktoria, shughuli zao kuu za kiuchumi ni uvuvi na biashara.

Wasweta huzungumza Kisweta na wamepakana na Wasurwa, Wahacha na Wasimbiti.

Eneo lao la makazi huitwa "Busweta" na Wasweta walio wengi ni waumini wa dini ya Kiislamu.

Njia zao za usafiri ni maji na barabara, Hutumia njia ya maji kupitia Ziwa Viktoria hadi Musoma mjini kwa kutumia boti, na gari hadi Tarime na Shirati ikiwa ndiyo miji ya jirani kwao.

Wasweta wanasifika kwa ukarimu na upole wao.

Jina la kabila linatokana na matunda yanayoitwa sweta: waanzilishi wa kabila hili wakati wanahama kutoka kusini mwa nchi ya Uganda, walifika sehemu ambayo walishikwa na njaa ikapelekea wao kula matunda ya mti wa sweta.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasweta kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.