Wikipedia:Makala ya wiki/WikiIndaba 2017

Logo ya WikiIndaba 2017

Wikiindaba 2017 ilikuwa mkutano wa taasisi ya Wikimedia Foundation kwa ajili ya Afrika uliofanyika mjini Accra (Ghana) tarehe 10 - 22 Januari 2017. Waliokaribishwa walikuwa wachangiaji wa Wikipedia pamoja na miradi mingine ya maaarifa huria kutoka nchi za Afrika pamoja na maafisa wa ofisi kuu ya Wikimedia. Shabaha ilikuwa kuimarisha mawasiliano kati ya washiriki na hali ya media huria barani Afrika.

Jina

WikiIndaba ni neno lililoundwa na "Wiki" kwa "Wikipedia / Wikimedia" na "Indaba" ambalo ni neno la lugha la Kizulu yenye maana ya "mkutano, ushauri wa pamoja'. Ilikuwa WikiIndaba ya pili baada ya mkutano wa kwanza uliotokea Afrika Kusini mwaka 2014.

Waliohudhuria

Kwa jumla walihudhuria mkutanoni watu 50 kutoka nchi 13 za Afrika (Afrika Kusini, Algeria, Botswana, Côte d'Ivoire, Ghana, Kamerun, Kenya, Moroko/Uswidi, Misri, Namibia, Nigeria, Tunisia, Uganda), mjumbe wa Wikipedia ya Kiswahili pamoja na Wageni kutoka Wikimedia Ujerumani na maafisa wa Wikimedia kutoka Marekani. Wageni wengine walitoka miradi ya maaarifa huria kama vile KIWIX na miradi ndani ya wikimedia kama vile Wiki Loves Africa, Wiki Loves Women, WikiFundi (programu za kuhariri wikipedia bila intaneti). ►Soma zaidi