Wilaya ya Gucha (pia: Wilaya ya Kisii Kusini au Wilaya ya Ogembo) ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Nyanza wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba ya katiba mpya ya nchi (2010). Jina limetokana na mto Gucha

Bonde la Ziwa Victoria huko Kenya OSM Wilaya ya Gucha'

Makao makuu yalikuwa Ogembo, yenye wakazi zaidi ya elfu moja na wageni zaidi ya elfu moja ambao huitembelea kila siku.

Kwa sasa imekuwa kaunti ndogo ya kaunti ya Kisii ikiwa na South Bogirango Gucha North Bogirango.

Wakazi wake walikuwa takriban 461,000 (1999) [1]. Idadi kubwa ya watu ni Wakisii, lakini hupakana na ardhi ya Wamasai huko kusini-mashariki. Kumekuwa na mapigano kadhaa ya kikabila baina yao.

Kilimo ndiyo sekta kuu. Mbali ya mashamba mengi madogo madogo, kuna mashamba makubwa ya miwa.

Wilaya hii ilikuwa na majimbo matatu: South Mugirango, Bomachoge na Bobasi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 viti vyote vitatu vilishindwa na chama cha Ford-People.

Mamlaka za Mitaa (Halmashauri)
Mamlaka Aina Idadi ya Watu Wakazi wa mjini*
Ogembo Jiji 48.725 1.654
Nyamarambe Jiji 40.232 212
Nyamache Jiji 38.924 2.205
Tabaka Jiji 26.325 5.067
Gucha County 306.733 1.946
Jumla -- 460.939 11.084
* 1999 census. Source: [2]
Maeneo ya utawala
Tarafa Idadi ya Watu Wakazi wa mjini* Makao makuu
Etago 59.652 0
Kenyenya 92.641 1.857
Nyacheki 56.998 405
Nyamache 54.722 1.702
Nyamarambe 67.060 3.850
Ogembo 78.827 1.465 Ogembo
Sameta 51.039 0
Jumla 460.939 9.279 --
* 1999 census. Sources: [3], [4],

Marejeo

hariri
  1. [1] Ilihifadhiwa 21 Mei 2005 kwenye Wayback Machine.

Viungo vya nje

hariri