Lindi (mji)
Lindi ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Lindi ikiwa na halmashauri yake ya kujitegemea kama wilaya ya pekee. Msimbo wa posta ni 651 . Lindi iko mdomoni wa mto Lukuledi takriban 150 km kaskazini ya Mtwara mwambaoni wa Bahari Hindi. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 41,549 [1]
Lindi | |
Mahali pa mji wa Lindi katika Tanzania |
|
Majiranukta: 9°59′49″S 39°42′52″E / 9.99694°S 39.71444°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Lindi |
Wilaya | Lindi Mjini |
Historia
haririLindi ilikuwa kati ya miji ya Waswahili wa kale katika pwani ya Bahari ya Hindi. Mdomo wa Lukuledi ulikuwa bandari nzuri kwa ajili ya jahazi za Waswahili na pia kwa meli ndogo za zamani za ukoloni. Siku hizi hautoshi tena kwa meli kubwa.
Wakati wa ukoloni wa Wajerumani ilikuwa makao makuu ya kusini-mashariki ya Tanzania bara. Ilikuwa kituo cha posta na pia cha kikosi na. 3 cha jeshi la Kijerumani. Ilibaki kitovu cha kusini wakati ya Waingereza hadi kujengwa kwa bandari ya Mtawara. Mazao ya kibiashara yalikuwa hasa katani baadaye pia korosho.
Maendeleo ya Lindi ilikwama kutokana na hali mbaya za barabara amabazo hazikutunzwa vizuri wakati wa uhuru. Kuna matumaini ya kwamba barabara mpya ya lami ya Dar es Salaam - Mtwara italeta nafasi mpya kwa maendeleo ya mji na mazingira yake.
Tazama pia
haririMarejeo
haririKata za Wilaya ya Lindi Mjini - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Chikonji | Jamhuri | Kilangala | Kilolambwani | Kitomanga | Kitumbikwela | Kiwawa | Makonde | Matimba | Matopeni | Mbanja | Mchinga | Mikumbi | Milola | Mingoyo | Mipingo | Mitandi | Mnazimmoja | Msinjahili | Mtanda | Mvuleni | Mwenge | Nachingwea | Nangaru | Ndoro | Ng'apa | Rahaleo | Rasbura | Rutamba | Tandangongoro | Wailes
|