Wiliamu wa York (mwishoni mwa karne ya 11York, Uingereza, 8 Juni 1154) alikuwa askofu wa York, Uingereza kuanzia mwaka 1141 hadi 1147, tena kuanzia 1154 hadi kifo chake kilichosemekana kusababishwa na sumu iliyotiwa katika kikombe cha ekaristi[1]

Wiliamu wa York akivuka mto Ouse pamoja na umati; daraja lilibomoka bila mtu yeyote kuumia.

Mtu mpole na mpendevu, alipofukuzwa jimboni kinyume cha haki, alijiunga na wamonaki wa Winchester, na aliporudi alisamehe maadui na kupatanisha wananchi [2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Papa Honori III alimtangaza tasmi kuwa hivyo tarehe 18 Machi 1226.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Juni[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Emma J. Wells, "Making Sense of Things", History Today, Vol. 69, No. 5 (May 2019), p. 40.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/56450
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Burton, Janet (1994). Monastic and Religious Orders in Britain: 1000–1300. Cambridge Medieval Textbooks. Cambridge UK: Cambridge University Press. ISBN 0-521-37797-8.
  • Burton, Janet (2004). "William of York (d. 1154)". Oxford Dictionary of National Biography. Oxford University Press. doi:10.1093/ref:odnb/9606
     . http://www.oxforddnb.com/view/article/9606. Retrieved 17 March 2008.

Marejeo mengine

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.