Yoana Delanoue (Saumur, Anjou, 18 Juni 1666 - Fencet, 17 Agosti 1736), alikuwa mtawa mwanzilishi wa Shirika la Mt. Ana wa Maongozi ya Mungu huko Ufaransa.

Mt. Yoana alivyochorwa.

Ingawa alikuwa na ubinafsi mkubwa tangu utotoni, alipoongoka akawa na upendo wa ajabu kwa maskini na tumaini kubwa kwa Maongozi ya Mungu hata akapokea nyumbani mwake mayatima, wajane, wagonjwa na makahaba akavuta wengine kuwahudumia pamoja naye[1].

Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Pius XII tarehe 8 Novemba 1947, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II 31 Oktoba 1982.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.