Yohane Boste
Yohane Boste (Dufton, Westmorland, Uingereza, 1544 hivi – Dryburn, Durham, 24 Julai 1594) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki mwaka 1576 akiwa mwalimu mkuu tayari.
Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, akapewa daraja ya upadri huko Reims (Machi 1581).
Mwezi uliofuata alirudi Uingereza na kufanya utume wake kwa siri hadi aliposalitiwa na kukamatwa mwaka 1593. Mwaka uliofuata alinyongwa na kukatwa vipandevipande akiwa bado hai.
Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.
Tazama piaEdit
TanbihiEdit
MarejeoEdit
Viungo vya njeEdit
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |