Yohane wa Pian del Carpine

Yohane wa Pian del Carpine (Magione, Perugia, 1185 hivi [1]1 Agosti 1252) alikuwa Mfransisko wa Italia aliyepata umaarufu kutokana na safari yake barani Asia.

Safari ya Yohane kwenda Mashariki inaonyeshwa kwa buluu namna ya reli.

Maisha

hariri

Baada ya kueneza shirika lake Ujerumani, alitumwa na Papa kama balozi kwa Khan mkuu wa Dola la Mongolia.[2] Yeye na wenzake walitembea kilometa 4,800 kwa siku 106.

Akiwa wa kwanza kufika huko aliandika kitabu cha kumbukumbu za safari yake kupitia Ukraina, Asia ya Kati na maeneo mengine ya dola hilo.

Alifanywa askofu mkuu wa Antivari, Montenegro, mwaka 1247.

Maandishi

hariri

Ystoria Mongalorum iliandikwa naye katika miaka ya 1240. Ndicho kitabu cha kwanza cha Wazungu kuhusu Wamongolia.[3]

Tanbihi

hariri
  1. "um 1185" in Mittelalter Lexikon: "Johannes de Piano Carpini" Archived 17 Septemba 2017 at the Wayback Machine..
  2. Montalbano, Kathryn A. (2015). "Misunderstanding the Mongols: Intercultural Communication in Three Thirteenth-Century Franciscan Travel Accounts". Information & Culture. 50 (4): 588–610. doi:10.7560/IC50406.
  3. Carpini, Giovanni; Hildinger, Erik (Aprili 27, 2014). The Story of the Mongols: Whom We Call the Tartars (tol. la 2nd). Branden Books. ISBN 0828320179.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.