Yohane wa Siracusa
Yohane wa Siracusa (Sicilia, karne ya 6 - Siracusa, leo nchini Italia, 609 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 593 hadi kifo chake.
Kabla ya hapo alikuwa shemasi mkuu wa Catania. Papa Gregori I alimteua ili kumpa Masimiano wa Siracusa mwandamizi wa kufaa. Pia alimsifu kwa mwenendo wake mwadilifu, kwa kujali haki, kwa busara, kwa ushauri nasaha na kwa uwajibikaji katika majukumu ya Kanisa[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |