Sirakusa (kwa Kiitalia: Siracusa, kwa Kiingereza:Syracuse) ni mji wa Italia uliopo kwenye pwani ya mashariki ya kisiwa cha Sisilia. Kwa karne nyingi tangu zamani za Ugiriki wa Kale Sirakusa ilikuwa mji mkuu wa Sisilia ikahesabiwa pia kati ya miji muhimu na yenye enzi ya dunia.

Sehemu ya mji wa Siracusa


Siracusa
Siracusa is located in Italia
Siracusa
Siracusa

Mahali pa Siracusa katika Italia

Majiranukta: 37°05′00″N 15°17′00″E / 37.08333°N 15.28333°E / 37.08333; 15.28333
Nchi Italia
Mkoa Sisilia
Wilaya Siracusa
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 124,453
Tovuti:  http://www.comune.siracusa.it/
Sirakusa - uwanja wa maigizo wa kale
Sirakusa - viwanda

Tangu 2005 Sirakusa imeandikwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.

Jiografia

hariri

Mji uko upande wa mashariki-kusini wa Sisilia. Idadi ya wakazi ni kama 124,000.

Kitovu cha kihistoria kipo kwenye kisiwa cha Ortygia kilichopo karibu sana na pwani yenyewe.

Historia

hariri

Jina la Sirakusa latokana na "Syrakka" inayomaanisha "matope".

Mji ulianzishwa mwaka 734 KK na walowezi Wagiriki kutoka Korintho kwenye kisiwa cha Ortygia kwa jina la "Syrakusai" (kwa Kigiriki Συράκουσαι). Mji ulikua haraka na kupanuka hadi Sisilia bara ukawa mji mkubwa wa Wagiriki katika Sisilia.

Ukitawaliwa na wafalme wake mji ulitunza uhuru wake kwa karne kadhaa. Sirakusa ilikuwa kitovu cha utamaduni na sayansi. Mshairi Aischylos, mwanafalsafa Platoni na mwanahisabati Archimedes waliishi hapa.

Mwaka 212 KK wakati wa vita ya pili ya Wapuni jeshi la Dola la Roma lilifaulu kuteka pia Sirakusa na kulifanya mji mkuu wa jimbo la Sisilia.

Mwaka 450 ilivamiwa na Wavandali na tangu 535 ilikuwa chini ya Bizanti.

Tangu 831 Waarabu Waislamu walishambulia na kuteka sehemu mbalimbali za Sisilia, mwishowe (878) pia Sirakusa.

Tangu 1038 ilirudi tena chini ya utawala wa Kikristo kwanza wa Wanormandi halafu chini ya makaisari wa Dola Takatifu la Kiroma.

Kutoka hapo iliingia chini ya utawala wa Kihispania, halafu ya ufalme wa Sisilia hadi kuingia katika nchi ya Italia mwaka 1860.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Siracusa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.