Yusufu
Yusufu ni jina la kiume lenye asili ya Kiebrania, linalotumiwa sana katika Biblia, kama יוֹסֵף, Yossef au Yôsēp̄.
Kwa Kiarabu, kwa mfano katika Qur'an, jina hilo linaandikwa يوسف, Yūsuf.
Kwa Kiswahili jina linatumika kwa kutamka Yosefu (hasa kati ya Wakristo) au Yusufu (hasa kati ya Waislamu), mbali na wale wanaotumia jina kwa matamshi ya Kiingereza, Joseph.
Mwanamke anaweza kuitwa Yosefa, Yosefina, Josefina.
Asili na maana
haririJina linaweza kutafsiriwa kutokana na יהוה להוסיף YHWH Lhosif, ambayo maana yake ni "Bwana aongeze". Ni maneno ya Raheli alipojaliwa hatimaye kumzaa mwanae wa kwanza: Yosefu (babu), mtoto wa 11 wa Yakobo Israeli.
Kutoka kwake lilipatikana kabila kubwa lililogawanyika kati ya lile la Manase na lile la Efraimu
Katika Agano Jipya, Yosefu ni hasa Yosefu (mume wa Maria), mama wa Yesu.
Mwingine ni Yosefu wa Arimataya, tajiri wa baraza la Israeli, aliyemzika Yesu.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |