Yosefu wa Kopertino
Yosefu wa Kopertino (Copertino 17 Juni 1603 – Osimo 18 Septemba 1663) alikuwa padri wa utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali.
Mtu wa sala hasa, alijaliwa karama za pekee, hasa ile ya kuelea hewani kwa muda mrefu wakati wa kutoka nje ya nafsi. Jambo hilo lilimsababishia matatizo mengi aliyoyavumilia vizuri, akizidi kung'aa kwa unyenyekevu, ufukara na upendo kwa waliomtamani Mungu[1].
Alitangazwa na Papa Benedikto XIV kuwa mwenye heri tarehe 24 Februari 1753, halafu Papa Klement XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- "Saint Joseph Copertino," Father Angelo Pastrovicchi, O.M.C., TAN Books and Publishers, 1980, ISBN 0-89555-135-7
Viungo vya nje
hariri- Essay from "Saints for Sinners" Ilihifadhiwa 13 Septemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia: St. Joseph of Cupertino
- Joseph of Cupertino Ilihifadhiwa 13 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine.
- St Joseph of Cupertino Ilihifadhiwa 21 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
- St Joseph of Cupertino Parish, Cupertino, California Ilihifadhiwa 23 Februari 2022 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |