Yterbi
Yterbi (Ytterbium) ni elementi ya kimetali yenye alama Yb na namba atomia 70, maana yake kiini cha Yterbi kina protoni 70 ndani yake. Uzani atomia ni 173.045. Katika jedwali la elementi inahesabiwa kati ya lanthanidi na metali za ardhi adimu.
Yterbi (Ytterbium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Yterbi (Ytterbium) |
Alama | Tb |
Namba atomia | 70 |
Mfululizo safu | Lanthanidi |
Uzani atomia | 173.045 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 8, 2 |
Densiti | 6.90 g/cm3 |
Kiwango cha kuyeyuka | °K 1097 |
Kiwango cha kuchemka | °K 1469 |
Kiasili Yterbi haipatikani kwa hali safi lakini imo ndani ya madini mengi.
Iligunduliwa mnamo mwaka 1878 wakati mwanakemia Mswisi Jean Charles Galissard de Marignac alitenga kutoka ardhi adimu ya "erbia" na kuiita Ytterbia kutokana na kijiji cha Ytterby, Uswidi ambako aliwahi kupata madini aliyochungulia.[1] [2]
Yterbi ni vigumu kutengwa na madini mengine, kwa hiyo haina matumizi mengi isipokuwa viwango vidogo katika leza kadhaa.
Marejeo
hariri- ↑ Mbali na Yterbi (Yb), kuna pia elementi za Ytri (Y), Erbi (Er) na Terbi (Tb) zilizopokea jina kutokana na kijiji cha Ytterby; elementi za Scandi (Skandinavia), Holmi (Ho, jina la Stockholm), Thuli (Tm, jina la Thule, kisiwa cha kaskazini katika mitholojia ya Kigiriki) ya Scandinavia), na Gadolini (Gd, jina la mvumbuzi Johan Gadolin) zilitambuliwa pia katika madini ya Ytterbi.
- ↑ Kean, Sam (16 Julai 2010). "Ytterby: The Tiny Swedish Island That Gave the Periodic Table Four Different Elements". Slate. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Kusoma zaidi
hariri- Guide to the Elements – Revised Edition, Albert Stwertka, (Oxford University Press; 1998) ISBN 0-19-508083-1
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yterbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |