Zinki ni elementi yenye namba atomia 30 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.409. Alama yake ni Zi.

Zinki (zincum)
Zinki
Zinki
Jina la Elementi Zinki (zincum)
Alama Zn
Namba atomia 30
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 65.409
Valensi 2, 8, 18, 2
Densiti 7.14 g/cm³
Ugumu (Mohs) 2.5
Kiwango cha kuyeyuka 692.68 K (419.53°C)
Kiwango cha kuchemka 1180 K (907 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.01 %
Hali maada mango

Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi ya buluu-nyeupe. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,180 .

Hupatikana ndani ya madini, haitokei kiasili kama elementi tupu. Huchimbwa hasa China, Peru, Australia, Kanada, Marekani, Meksiko na Afrika Kusini.

Mabati ya paa huhitaji zinki.

Matumizi ya zinki ni takriban tani milioni 11 (kwa mwaka 2006). Takriban nusu yake ni kwa kuzuia ubabuzi (kutokea kwa kutu) wa mabati au vifaa vingine vya chuma kwa njia ya galvania n.k..

Vinginevyo hutumiwa katika aloi kama shaba nyeupe na hasa kutengeza betri.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zinki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.