Ziwa Great Slave (kwa Kifaransa: Grand lac des Esclaves; kwa Kiingereza: Great Slave Lake) ni ziwa la pili kwa ukubwa katika maeneo ya Northwest Territories ya Kanada. Ni ziwa lenye kina kirefu zaidi katika Amerika Kaskazini likifikia mita 614 [1] na ziwa kubwa la tisa duniani. Urefu wake ni km 480 likiwa na upana wa km 19 hadi 109, hivyo kuwa na eneo la km2 27,200.

Ziwa Great Slave
Ufuko wa mashariki
Ufuko wa mashariki
Nchi zinazopakana Kanada, jimbo la Northwest_Territories
Eneo la maji km2 27,200
Kina cha chini m 614
Mito inayoingia Mito ya Hay, Slave, Taltson, Lockhart, Yellowknife
Mito inayotoka Mto Mackenzie
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
m 156

Jina linatokana na neno la utani la Maindio wa Cree kwa maadui wao waliokalia sehemu ya ziwa. Waliwaita "watumwa" na jina hili lilitafsiriwa na Wafaransa wa kwanza waliofanya biashara na Wacree na kuingizwa katika ramani zao wakiandika "Lac des Esclaves" (ziwa la Watumwa, walishika pia "mto wa watumwa"). Umbo hili la Kifaransa lilitafsiriwa baadaye kwa Kiingereza "Slave Lake", ilhali kuna "Great Slave Lake" na "Lesser Slave Lake", pia "Slave River".

Miji kwenye ziwa ni pamoja na: Yellowknife, Hay River, Behchoko, Fort Resolution, Lutselk'e, Hay River Reserve, Dettah na N'Dilo.

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Hebert, Paul (2007). "Encyclopedia of Earth". Washington, DC: Environmental Information Coalition, National Council for Science and the Environment. Iliwekwa mnamo 2007-12-07. 

Tovuti za Nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Great Slave kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.