Zodiaki
Zodiaki ni kanda kwenye anga zenye upana wa takriban nyuzi 20 zinazofuata mstari wa njia ya Jua yaani mstari wa njia dhahiri ya Jua angani katika mwendo wa mwaka mmoja. Mstari huo unapatikana kwa kutazama Jua wakati wa mapambazuko ambako linaonekana katika mazingira ya makundinyota tofauti. Kila mwaka Jua linapambazuka katika eneo la makundinyota yaleyale.
Njia dhahiri za Mwezi na sayari zinaonekana pia katika kanda hii ya zodiaki.
Hadi leo unajimu unatumia makundinyota 12 kama buruji za falaki kwa imani ya kwamba nyota hizi zina athari kwa kipindi fulani cha mwaka kinachoitwa kufuatana na kundinyota au buruji ya falaki yake. Lakini hali halisi Jua linapita katika maeneo ya makundinyota 13, si 12.
Miaka 3000 iliyopita, ambapo mfumo wa Zodiaki ulibuniwa, wataalamu wa Babeli waliondoa kundinyota la Hawaa (Ophiuchus) katika mfumo kwa shabaha ya kupata mgawanyo wa anga unaolingana na miezi 12 ya kalenda.
Kumetokea pia badiliko la kwamba makundinyota ya Zodiaki hayalingani tena na vipindi vya mwaka ambapo yanatangazwa na wanajimu wa leo. Sababu yake ni kusogea kwa mhimili wa Dunia na hii inasababisha ya kwamba sisi tunatazama anga kwa pembe tofauti kuliko wazee miaka 2000 iliyopita. Ila tu wanajimu wanaendelea kutumia vipindi vilivyopimwa zamani zile.
Makundinyota ya ekliptiki
haririJedwali lifuatalo linaonyesha hali halisi ya makundinyota 13 yanayopitiwa na Jua katika mwendo wa mwaka mmoja. Kwa sasa nukta ya machipuo iko ndani ya Hutu (Pisces) hivyo hapa iko nafasi ya 0°
Kundinyota | Ishara | Nafasi kwenye ekliptiki |
Kipindi cha kupita kwa Jua (mwaka 2010) |
Kipindi cha Buruji ya Falaki inayolingana katika unajimu | |
---|---|---|---|---|---|
Kiswahili | Kilatini | ||||
Kondoo (Hamali) | Aries | 28,8°–53,5° | 19. Apr – 14. Mei | 21 Machi- 19 Aprili | |
Ng'ombe (Tauri) | Taurus | 53,5°–90,2° | 14 Mei – 21 Juni | 20 Aprili – 21 Mei | |
Mapacha (Jauza) | Gemini | 90,2°–118,1° | 21 Juni– 20. Julai | 22 Mei – 20 Juni | |
Kaa (Saratani) | Cancer | 118,1°–138,2° | 20 Julai – 11. Agosti | 21 Juni – 22 Julai | |
Simba (Asadi) | Leo | 138,2°–173,9° | 11 Agosti – 17. Sept | 23 Julai – 22 Agosti | |
Mashuke (Nadhifa) | Virgo | 173,9°–218,0° | 17 Sept – 31 Okt | 23 Agosti – 22 Sept | |
Mizani | Libra | 218,0°–241,0° | 31 Okt – 23 Nov | 23 Sept – 23 Okt | |
Nge (Akarabu) | Scorpius | 241,0°–247,7° | 23 Nov – 30 Nov | 24 Okt – 21 Nov | |
Hawaa | Ophiuchus | 247,7°–266,3° | 30 Nov – 18 Des | (ilipunguzwa katika unajimu) | |
Mshale (Kausi) | Sagittarius | 266,3°–299,7° | 18 Des – 20 Jan | 22 Nov – 21 Des | |
Mbuzi (Jadi) | Capricornus | 299,7°–327,6° | 20 Jan – 16 Feb | 22 Des – 19 Jan | |
Ndoo (Dalu) | Aquarius | 327,6°–351,6° | 16 Feb – 12 Machi | 20 Jan – 18 Feb | |
Samaki (Hutu) | Pisces | 351,6°–28,8° | 12 Machi – 19 Apr | 19 Feb – 20 Machi |
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
Makundinyota ya Zodiaki Majina ya kisasa yanafuatwa kwa mabano na jina la mabaharia na jina la Kilatini (la kimataifa) |
||
---|---|---|
Kaa (Saratani – Cancer ) • Kondoo (Hamali – Aries ) • Mapacha (Jauza – Gemini ) • Mashuke (Nadhifa – Virgo ) • Mbuzi (Jadi – Capricornus ) • Mizani – Libra ) • Mshale (Kausi – Sagittarius ) • Ndoo (Dalu – Aquarius ) • Nge (Akarabu – Scorpius ) • Ng'ombe (Tauri – Taurus ) • Samaki (Hutu – Pisces ) • Simba (Asadi – Leo ) |