Ndui ya nyani (kwa Kiingereza: monkeypox) ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unafanana na ndui ya kawaida iliyokwishakomeshwa, ila si mkali hivyo. Kuna wataalamu walioanza kukosoa matumizi ya jina hilo kama udanganyifu, kwa sababu ugonjwa huo, hata kama ulikuwa wa wanyama wa aina hiyo kwanza, sasa kwa kawaida unaambukizwa na binadamu kwa binadamu mwenzie, hasa kwa njia ya shahawa.

Dalili za ndui ya nyani katika ngozi.
Mlipuko wa ndui ya nyani kwa nchi
Pinki iliyoiva - Kladi ya Afrika ya Magharibi
Buluu - Kladi ya Afrika ya Kati
Zambarau - Kladi zote mbili zimeripotiwa
Nyekundu - Mlipuko wa 2022 nje ya eneo la kawaida
Pinki - Visa vituhumiwavyo

Chanzo chake ni virusi vinavyoambukizwa kwa ujirani wa muda mrefu kidogo. Chanjo ya ndui ilikuwa inasaidia kukinga dhidi ya aina hiyo pia, lakini baada ya ugonjwa huo kwisha na chanjo kusimamishwa, kingamwili ya wengi imepungua.

Uenezi hariri

Mapema Mei 2022, visa vya ndui ya nyani viligunduliwa katika watu nje ya maeneo ya Afrika ilipozoeleka, hasa nchini Uingereza, Uhispania, Ureno, Kanada na Marekani, [1] kisha Italia, Uswidi, Ubelgiji, Ufaransa, Australia na Ujerumani na nchi nyingine 70 [2].

Imegundulika kwamba maambukizi mengi kati ya hayo ya kwanza yametokea katika sherehe ya kimataifa ya mashoga iliyofanyika Madrid, lakini habari hiyo imezuiwa kutangazwa isije ikachochea unyanyapaa dhidi yao [3]. Hofu hiyo imechangia kufanya maradhi yazidi kuenea katika nchi nyingi zaidi hata yakatangazwa na Shirika la Afya Duniani kuwa tishio la kimataifa linalohitaji ushirikiano wa wote, kwanza kwa kutoa taarifa kamili kwa umati [4].

Waliopatwa kwa asilimia 98 ni mashoga[5]. Baadhi yao wameshafariki dunia[6][7][8][9][10].

Uchunguzi wa filojenetiki ya virusi husika ulionyesha kuwa ni mwana wa kladi ya Afrika ya Magharibi. [11]

Tanbihi hariri

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndui ya nyani kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.