Milima Air
(Elekezwa kutoka Aïr)
Aïr (tamka: a-ir) ni safu ya milima katika nchi ya Niger (Afrika).
Urefu wake unafikia hadi mita 2,022 juu ya usawa wa bahari. Eneo la Air ni kilomita za mraba 84,000. Milima hii iko katikati ya jangwa la Sahara na kutokana na kuinuliwa juu ya mazingira ya jangwa ina tabia kama kisiwa chenye tabianchi tofauti. Hata kama usimbishaji ni mdogo, kimo chake hupunguza joto na kinatunza kiwango cha unyevu kilichopo juu ya jangwa na hivyo kuruhusu kuwepo kwa uoto tofauti na jangwa.
Tazama pia
hariri
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milima Air kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |