Abdulrahman Omari Kinana
Abdulrahman Omari Kinana (alizaliwa 1951) ni mwanasiasa Mtanzania aliyewahi kuhudumu katika Bunge la Afrika Mashariki kama spika wa Bunge hilo kutoka mwaka 2001 hadi 2006.[1]
Abdulrahman Kinana | |
Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi
| |
Muda wa Utawala Novemba 2012 – Mei 2018 | |
Mwenyekiti | John Pombe Magufuli |
---|---|
mtangulizi | Wilson Mukama |
Spika wa kwanza wa EALA
| |
Muda wa Utawala Novemba 2001 – 2006 | |
aliyemfuata | Abdirahim Abdi |
tarehe ya kuzaliwa | 1951 |
utaifa | Tanzania |
chama | CCM |
Alikuwa katibu mkuu wa chama tawala, aliyepambana sana katika kipindi kigumu ndani ya Chama cha Mapinduzi, kutoka mwaka 2012 mpaka hapo alipojiuzulu mwaka 2018.[2] Mwaka 2022 alichaguliwa kwa kauli moja kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Tanzania bara.
Kinana, mwenye asili ya Somalia, aliwahi kutumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka ishirini akiwa na cheo cha Kanali mnamo mwaka 1972.
Alishawahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM jimbo la Arusha kwa muda wa miaka 10. Alishawahi kuwa Naibu waziri wa Wizara ya ulinzi, na wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
Tanbihi
hariri- ↑ "Profile: Kinana". East African Legislative Assembly. Iliwekwa mnamo 19 Mei 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://peoplepill.com/people/riziki-said-lulida/
Viungo vya nje
hariri- https://www.youtube.com/watch?v=xy4kFIgSc98
- Keynote address by Kinana at Carleton University katika YouTube
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Abdulrahman Omari Kinana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |