Agabo (kwa Kigiriki Ἄγαβος, Agabos) alikuwa mmojawapo kati ya Wakristo wa kwanza kati ya Palestina na Siria.

Utabiri wa Agabo kadiri ya Louis Cheron (1660-1713).

Anatajwa mara mbili na kitabu cha Matendo ya Mitume kama nabii aliyeongozwa na Roho Mtakatifu[1].

Agabo anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu mbalimbali ya Ukristo.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Februari, 8 Machi au 8 Aprili[2][3].

Habari zake

hariri

Kadiri ya Mdo 11:27-28, alikuwa mmoja wa manabii waliofika Antiokia kutoka Yerusalemu na alitabiri njaa kali iliyotokea duniani kote wakati wa kaisari Klaudio.

Kadiri ya Mdo 21:10-12, miaka mingi baadaye (58 hivi BK), Agabo alikutana na Mtume Paulo huko Kaisarea Maritima akamtabiria atakavyokamatwa mapema na kuteswa na watu wa mataifa.

Kadiri ya mapokeo alikuwa mmojawapo kati ya wanafunzi 70/72 wa Yesu na alifia dini huko Antiokia, lakini hakuna hakika yoyote[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Agabo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.