Ajali ya Ndege ya Ethiopia 302

Ndege ya Ethiopia 302 (Ethiopian Airlines Flight 302) ilikuwa ndege ya kimataifa iliyokuwa imepangiwa safari yake kutoka Bole International Airport ya Addis Ababa, Ethiopia, kwenda Jomo Kenyatta International Airport ya Nairobi, Kenya ambapo mnamo 10 Machi 2019 ndege hiyo ilidondoka na kulipuka, hivyo kusababisha vifo vya watu wote 157 (abiria, wahudumu na marubani) waliokuwemo ndani yake.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni muda mfupi tu ambapo tukio la kufanana na hilo lilitokea mnamo Oktoba 2018 huko Lion Air Flight 610 Jakarta, Indonesia ambapo ndege ya Boeing 737 MAX 8 (Lion Air Flight 610) ilidondoka muda mchache baada ya kupaa.

Ajali hii inatajwa kuwa ndiyo ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa ndege za Ethiopia ambapo ajali hii imelizidi tukio la utekaji wa ndege ya Ethiopia 961 Ethiopian Airlines Flight 961 tukio lililotokea mwaka 1996 huko Komoro, pia ajali hii inatajwa kuwa ndiyo ajali mbaya zaidi kuwahi kuua abiria wengi kwa ndege za Ethiopia.[1] [2] [3] [4]

[5]

Ajali hariri

Ndege ya Ethiopia 302 ilibeba watu kutoka mataifa 33 tofauti, wakiwemo wasafiri 149 na kikosi cha waongoza ndege 8 na kufanya jumla ya watu ndani ya ndege hiyo kufikia 157.[6] Baada ya rubani wa ndege hiyo kuripoti kuwa kulikuwa na tatizo kwenye ndege hiyo, mara ndege hiyo ilipotea kwenye mtambo wa rada wa kuongozea ndege na dakika sita baada ya kupaa ilianguka.[7]

Ndege hiyo ilidondoka jirani (kama km 62) na mji wa Bishoftu kusini mashariki mwa uwanja wa ndege wa Bole International Airport ambapo katika ajali hiyo hakuna aliyepona.[8]


Marejeo hariri